TANGAZO


Saturday, November 26, 2022

WAZIRI MHAGAMA AZINDUA BODI YA WAKURUGENZI YA KWANZA YA MAMLAKA YA SERIKALI MTANDAO (EGA)

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama akimkabidhi vitendea kazi Bw. Eric Shitindi ambaye ni mmoja wa Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Serikali Mtandao (eGA), mara baada ya Waziri huyo kuizindua bodi hiyo jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama akizungumza na Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Serikali Mtandao (eGA) jijini Dar es Salaam, mara baada ya ya Waziri huyo kuizindua bodi hiyo. 

Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Xavier Daudi akitoa neno la utangulizi kabla ya kumkaribisha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama kuzindua Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Serikali Mtandao (eGA).

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Serikali Mtandao (eGA), Dkt. Mussa Kissaka akitoa neno la shukrani kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama, mara baada ya Waziri huyo kuzindua Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Serikali Mtandao (eGA).

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Serikali Mtandao (eGA), Mhandisi Benedict Ndomba akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya eGA kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama wakati wa uzinduzi wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka hiyo.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama akiwa katika picha ya pamoja Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Serikali Mtandao (eGA), mara baada ya Waziri huyo kuizindua bodi hiyo jijini Dar es Salaam. Wa pili kutoka kulia ni Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI Bw. Xavier Daudi.

 

 

Na James Mwanamyoto, Dar es Salaam


WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama amewataka Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Serikali Mtandao (eGA) kusimamia vema utendaji kazi wa Serikali Mtandao ili kupunguza uwezekano wa wananchi kuathiriwa na vitendo vya rushwa.

 

Mhe. Jenista ametoa wito huo jijini Dar es Salaam, wakati akizindua Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Serikali Mtandao (eGA) ambayo imepewa jukumu la kuisimamia Mamlaka hiyo kuhakikisha inatekeleza wajibu wake.

 

Mhe. Jenista amesema matumizi ya serikali mtandao yanawaepusha wananchi kukutana na watendaji hivyo kuondoa mazingira yanayoshawishi vitendo vya rushwa.

 

Amewataka Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya eGA kuweka mikakati madhubuti na imara itakayoiwezesha Serikali Mtandao kutatua changamoto zinazowakabili wananchi pindi wanapofuata huduma mbalimbali katika Taasisi za Umma.

 

“Ninasisitiza wajumbe wa bodi mjikite zaidi katika kuhakikisha mnaweka mikakati ya matumizi ya TEHAMA ambayo itaondoa changamoto ya upatikanaji wa huduma hasa kwa wananchi wa kawaida ambao Mhe. Rais amedhamiria kuwapatia huduma stahiki,”

 

Naye, Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Xavier Daudi amesema kuwa, Wajumbe wa Bodi hiyo ya Wakurugenzi ya eGA wakitekeleza wajibu wao ipasavyo kwa kusimamia kikamilifu sera za serikali mtandao, wataisaidia Mamlaka ya Serikali Mtandao kulifikisha taifa katika uchumi wa kidijitali na mapinduzi ya nne ya viwanda, ikiwa ni pamoja na kuwezesha utekelezaji wa Dira ya Maendeleo ya Taifa ya mwaka 2025.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Serikali Mtandao (eGA), Dkt. Musa Kissaka amesema wajumbe wa bodi anayoiongoza wamepokea majukumu na maelekezo ambayo Mhe. Jenista ameyatoa, na kuahidi kuwa watajitahidi kadiri ya uwezo wao kufanya kazi kwa bidii na weledi katika kuisimamia na kuiongoza Mamlaka ya Serikali Mtandao.

 

Akizungumzia utekelezaji wa majukumu ya Mamlaka ya Serikali Mtandao, Mkurugenzi Mkuu wa mamlaka hiyo, Mhandisi Benedict Ndomba amesema, mamlaka anayoiongoza imeendelea kusimamia na kuhimiza uzingatiaji wa Sheria, Kanuni, Viwango na Miongozo ya Serikali Mtandao katika Taasisi za Umma.

 

Mhandisi Ndomba ameongeza kuwa, Mamlaka ya Serikali Mtandao imeendelea kufanya kaguzi za mifumo ya TEHAMA, kufuatilia usalama wa Serikali Mtandao ikiwa ni pamoja na kufanya tafiti na kutoa mafunzo ya Serikali Mtandao kwa watendaji wa Serikali.

2 comments:

  1. Ushuhuda Wangu wa Dhati 💖

    Baada ya baba yangu mdogo kuniacha kwa miezi saba ndefu, nilivunjika kabisa. Alinifungia kwenye mitandao yote ya kijamii, akasafiri mbali, na hakukuwa na njia ya kumfikia. Nilikaribia kukata tamaa juu yetu, lakini ndani kabisa nilijua singeweza kupata mtu yeyote ambaye angenipenda na kunitendea jinsi alivyonitenda.

    Siku moja, bosi wangu kazini aliona jinsi nilivyokuwa na huzuni na akanitambulisha kwa Dk. Dk. Dawn alisikiliza hadithi yangu na akaahidi kwamba mpenzi wangu atanirudia ndani ya siku tatu. Kusema kweli, sikuamini mwanzoni—lakini kwa mshangao mkubwa zaidi, siku ya tatu simu yangu iliita. Ilikuwa ni yeye! Alikuwa akilia na kuomba msamaha, akisema hataniacha tena.

    Tangu siku hiyo, uhusiano wetu umekuwa wenye nguvu na mzuri zaidi kuliko hapo awali. Amekuwa akinipenda na kunijali sana mimi na mtoto wetu, na sasa tunafunga ndoa baada ya miezi miwili tu! ❤️

    Shukrani zote kwa Dk. Dawn, ambaye kwa kweli aliwezesha jambo lisilowezekana. Ninampendekeza kwa moyo wote kwa yeyote anayekabiliwa na changamoto katika:

    Masuala ya mahusiano au ndoa

    Ugonjwa au magonjwa

    Ugumba au matatizo ya bahati nasibu

    Kesi za mahakama au kurejesha mali


    Dk. Dawn kweli hutatua matatizo kwa ufanisi na hurejesha furaha katika maisha ya watu.

    Wasiliana na Dr. Dawn kwenye WhatsApp: +2349046229159
    Barua pepe: dawnacuna314@gmail.com

    ReplyDelete
  2. Your Android car stereos really redefine smart driving. Having entertainment and navigation combined makes a huge difference. Excellent innovation! android car stereo systems

    ReplyDelete