Jarida la Forbes limewaorodhesha vijana wa Afrika mshariki wanotarajiwa kuwa mabilionea katika siku za usoni.
Vijana hao waliorodheshwa kulingana na teknolojia, bishara na ubunifu pia wanashirikisha, mwanamuziki wa Nigeria Davido.
Miongoni mwao ni raia wawili Kutoka Tanzania, wanne kutoka Kenya na mmoja kutoka Uganda.
Utafiti huo ulichunguza zaidi ya majina 600, ambayo yalikaguliwa kwa wiki kadhaa.
Walioorodheshwa walikuwa wafanyibiashara wenye mawazo mapya, ukubwa wa biashara zao, mapato yao, maeneo yaliopo, fursa walionayo, changamoto na mchango wao kwa jamii.
Jopo la majaji baadaye liliwajadili vijana 90 walioteuliwa. Pengine huwezi kuwatambua majina yao, sio matajiri lakini huenda wakawa mabilionea wa kesho.
Orodha ya vijana hao ni kama ilivyo:
1. Isaya Yunge, miaka 28, Tanzania
Mwanzilishi: kampuni ya teknolojia ya SomaApps
SomaApps ni kampuni ya programu inayowaunganisha wanafunzi na wadhamini wa elimu waliopo nchini na ugenini. Lengo lake ni kuharakisha ujio wa teknolojia za programu ya simu za mkononi, kutengeza roboti kuangazia mtandao wa Mambo ya Tanzania. Anaajiri watu 12.
2. Herieth Paul, miaka 22, Tanzania
Mwanamitindo
Paula aligunduliwa katika kampuni moja ya wanamitindo nchini canada. Aliajiriwa na kampuni ya Women Management mjini New York in 2010 na alionekana kuanza kupata ufanisi kuanzia hapo. Aliangaziwa katika jarida ya Vogue nchini Itali ambapo picha yake ilikuwa katika ukurasa wa juu wa jarida hilo. Ni miongoni mwa wanamitindo watatu katika kampeni ya majira ya baridi ya Tom Ford Fall/Winter 2013 akiwa amepigwa picha na mwenye mitindo mwenyewe. Pia alishiriki katika onyesho la mitindo la Victoria Secret Fashion mara mbili, na amejiunga na wanamitindo kama vile Gigi Hadid na Jourdan Dunn kama uso wa Maybelline.
3. Kevin Lubega, 28, Uganda
Mwazilishi: EzeeMoney
Ikianzishwa mwaka 2012, EzeeMoney ni kampuni ya kiteknolojia inayotoa huduma za fedha za kielecktroniki kwa wateja walio ama wasio na simu wala akaunti za benki na ambao wanaotaka kujipatia fedha na kufanya malipo fulani. Pia wanajitolea kulipia matumizi, hukusanya na kusafirisha fedha kwa mabenki na mashirika yasio na mabenki, serikali na mashirika yasio ya serikali.
EzeeMoney inafanya operesheni zake nchini Uganda, Kenya, Tanzania, Mozambique na Zimbabwe. Imewaajiri moja kwa moja watu 80 na wengine 8000 kwa njia isio moja kwa moja.
4.Leonida Mutuku, miaka 29, Kenya
Mwanzilishi: Intelipro
Mwaka 2015, Mutuku alianzisha kampuni ya Intelipro, kampuni inayotengeza programu zinazosaidia biashara kupokea data. Wateja wao ni kampuni ya MTN, Benki ya Africa nchini Ghana na Revoltura.
5. Huston Malande, miaka 28, Kenya
Mwanzilishi: Skyline Design
kampuni ya Skyline Design Ltd ni kampuni inayotengeza tovuti na bidhaa za wateja wa makampuni tangu 2008. Kwa sasa ina wafanyikazi sita wa kudumu na washuri 12 wenye kandarasi. Yeye na mshirika wake pia wameunda kundi la kampuni
Wengine ni kampuni ya Beiless Group ilioanzishwa mwaka 2015: Lengo lake ni kutoa huduma za matangazo, suluhu ya kiteknolojia kwa biashara. Huduma zake ni pamoja na kampeni za vyombo vya habari, usimamizi wa mitandao ya kijamii, mawasiliano ya kimkakati katika mitandao, matangazo ya kidijitali na uundaji wa maudhui. Wakenya wengine ni June Syowiana Leroy Mwasaru
No comments:
Post a Comment