TANGAZO


Wednesday, June 6, 2018

Akutana na mwanaye miaka 30 baada ya kuitoa mimba

Melissa Ohden

Haki miliki ya pichaMELISSA OHDEN
Image captionMadaktari walidhani Melissa ataishia kutoona na kwa wakati mmoja walihofia atashikwa na matatizo ya moyo
Akiwa na miaka 14, Melissa Ohden aliijuwa siri kubwa - mamake alijaribu kumuua akiwa angali tumboni.
Aliokolewa na mhudumu wa afya aliyemsikia akilia katika taka taka za hospitali nchini Marekani.
Hii ni hadithi ya uhai wake, na kuhusu mamake aliyedhani kwamba amekufa.
"Nili inukia nikijua kwamba nilizaliwa kabla ya kutimiza miezi 9, na kuwa niliasiliwa," Melissa Ohden, sasa ana miaka 41 anasema.
"Kitu ambacho sikujuwa ni kwamba kulikuwana siri kubwa. Kwamba nilitakiwa nife, na badala yake nilizaliwa nikiwa hai."
Mnamo 1977, katika hospitali moja nchini Marekani katika jimbo la Iowa, Mamake Melissa aliyekuwa na umri wamiaka 19 aliavya mimba kwa kutumia kemikali kwa zaidi ya siku tano.
Melisaa alizaliwa akiwana miezi minane akiwa na kilo 1.3 na akatupwa kwenye taka taka za hospitali.
Hapo ndipo nesi mmoja alisikia sauti ya mtoto akilia na kwa kuchungulia akaona mwili ukisogea.
Melissa alikimbizwa katika chumba cha wagonjwa mahututi ambapo aliponea na kuishi.
Melissa na dadakeHaki miliki ya pichaMELISSA OHDEN
Image captionMelissa na dadake
Madaktari walidhani atakuwa hawezi kuona na kwa wakati mmoja walidhani ataugua matatizo ya moyo yasiotibika.
Lakini amefanikiwa kuishi maisha yenye afya tele na amelelewa na familia iliomuasili.
Melissa - ambaye ameandika vitabu kuhadithia maisha yake- anasema aligundua kwamba aliasiliwa wakati alipogombana na dadake kutoka familia iliomuasili.
Kwa mara ya kwanza Melissa alichanganyikiwa, lakini wakati fahamu ilipomuingia na alipokaa kuzungumza na wazazi waliomlea hapo ndipo athari ikamjia kwa kuugua matatizo ya kiakili.
Uchungu uliendelea kuongezeka, mpaka miaka mitano baadaye - akiwa na miaka 19 - alichukuwa uamuzi wa kijasiri kumsaka mamake aliyetaka kumtoa uhai.
Ni shughuli iliyomchukua muda wa karibu muongo mmoja, lakini hatimaye alimpata - na akagundua ukweli ulimshutusha.
Melissa Ohden
Image captionMelissa akiwa na miaka 14 ndiyo alitambua kwa mara ya kwanza kuwa mamake alijaribu kumuavya
"Siri kubwa kweli ni kuwa mamangu alikaa miaka 30 akiamini kwamba nilifariki hospitalini.
"Hakuambiwa kwamba nilipona, ilikuwa siri aliofichwa," anasema.
Na ndio kwa sababu hiyo walipokutana ana kwa ana miaka mitatu baada ya kutumiana barua pepe, Melissa aliguswa na kwamba mamake alijutia kitendo hicho, kilichomsumbua roho kwa miaka mingi.
Lakini mshtuko haukumalizika hapo.
Mamake mzazi, Ruth, alimuambia kwamba hakutaka kuitoa mimba, na kwamba aliwekwa katika hali ambayo ni kama alilazimishwa kuitoa mimba hiyo.
"Nilichokuja kujua ni kwamba bibi yangu - mamake mamangu - alikuwa mhudumu maarufu wa afya katika jamii, na mtu anayefanya kazi ya kutoa mimba alikuwa na rafiki yake.
"Kwa pamoja walimlazimisha mamangu kinyume na ridhaa yake kuitoa mimba.
Melissa Ohden
Image captionMelissa Ohden amekutana na mamake kwa mara ya kwanza akiwa na miaka 30
Melissa anasema yeye ni "mojawapo ya watu wenye bahati duniani", kwanza kwamba aliweza kupona mkasa huo, na pia kubarikiwa na kuwa na wazazi waliomuasili na mamake mzazi katika maisha yake.
Kwa bahati tu, Melissa na mamake mzazi sasa wanaishi mjini Kansas pamoja na mojawapo wa dada zake wa kambo.

No comments:

Post a Comment