TANGAZO


Friday, December 8, 2017

Karibu watu 200,000 wakimbia moto wa nyika California

Flames leap along the 101 freeway in La Conchita, Ventura County, as a firefighter stands nearby on December 7, 2017

Haki miliki ya pichaAFP
Image captionKaribu watu 200,000 wakimbia moto wa nyika California
Karibu watu 200,000 kawa sasa wamehamishwa kufuatia moto wa nyika huko California huku makundi yakijaribu kuuzima moto huo.
Wazima moto 5,000 wamekuwa wakipambana na moto huo ambao umeharibu mamia ya nyumba kusini mwa jimbo la California.
Idadi ya watu waliohamishwa iliongezeka karibu mara nne siku ya Ijumaa baada ya moto wa tano kuzuka kaskazini mwa San Diego.
Firefighters remove a painting as they continue to extinguish fires in a home during the Haki miliki ya pichaEPA
Image captionWazima moto wakiondoa bidhaa kutoka kwa nyumba
Kifo kimoja kimeripotiwa hadi sasa baada ya mwanamke mmoja kupatikana eneo lililokuwa limeteketea katika kaunti ya Ventura.
Hadi Alhamisi jioni, idara ya moto ya California ilisema kuwa moto ulilazimu kuhamishwa kwa watu 189,000.
A huge plume of black smoke rises from a burning home on a hilltop beside one still standing in Bel Air, east of the 405 freeway on December 6, 2017 in Los Angeles, CaliforniaHaki miliki ya pichaAFP
Image captionNyumba nyingi zilizo kwenye hatari ni za mamilioni ya dola
Gavana wa California Jerry Brown ametangaza hali ya tahadharai eneo hilo.
Ikulu ya White House nayo inasema itatoa msaada wowote unaohitajika.
Upepo wenye joto wa Santa Ana wa jangwani umesababisha moto huo kuongezeka zaidi.

No comments:

Post a Comment