TANGAZO


Friday, December 8, 2017

BALOZI WA TANZANIA NCHINI SAUDI ARABIA, HEMEDI MGAZA ATEMBELEA TAASISI YA MOYO YA JAKAYA KIKWETE (JKCI) KUANGALIA MAANDALIZI YA KAMBI YA UPASUAJI MOYO INAYOTARAJIWA KUANZA JUMAPILI TAREHE 10/12/2017

Mkurugenzi Mtendaji wa  Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete  (JKCI) Prof. Mohamed Janabi (kulia) akiwa katika picha ya pamoja na  Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia Mhe. Hemedi Mgaza (wa pili kushoto) pamoja na Madaktari bingwa wa Magonjwa ya Moyo kwa watoto wa JKCI na Taasisi ya Little Hearts  ya nchini Saudi Arabia. Mhe. Balozi Mgaza alitembelea Taasisi hiyo leo kwa ajili ya kuangalia  maandalizi ya kambi ya upasuaji wa Moyo kwa watoto na watu wazima inayotarajia kuanza siku ya jumapili tarehe 10/12/2017. 
Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia Mhe. Hemedi Mgaza (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Madaktari bingwa wa Magonjwa ya Moyo kwa watoto  Naiz Majani na Ali Al-Akhfash wa Taasisi ya Little Hearts  ya nchini Saudi Arabia mara baada ya kumaliza ziara yake ya kutembelea JKCI kwa ajili ya kuangalia maandalizi ya kambi ya upasuaji wa Moyo kwa watoto na watu wazima inayotarajia kuanza siku ya jumapili tarehe 10/12/2017. Jumla ya wagonjwa 80 wanatarajia kufanyiwa upasuaji wa kufungua na bila kufungua kifua katika kambi hiyo.(Picha zote na JKCI)

TAASISI ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na Taasisi ya Little Hearts ambao wanafadhiliwa na Taasisi ya Al- Murtada ya nchini Saudi Arabia wanatarajia kufanya matibabu ya moyo kwa wagonjwa 80 katika kambi maalum inayotarajia kuanza tarehe 10 – 14/12/2017.
Matibabu yatakayofanyika katika kambi hiyo ni ya upasuaji wa kufungua kifua na upasuaji wa bila kufungua kifua (Catheterization) kwa kutumia  mtambo wa Cathlab kwa watoto na watu wazima.
Leo tarehe 08/12/2017 madaktari bingwa wa Moyo wameanza kufanya uchunguzi kwa wagonjwa wote watakaofanyiwa upasuaji. Katika kambi  hii  ya siku tano tumepanga kufanya upasuaji wa moyo kwa wagonjwa 30 na upasuaji wa bila kufungua kifua kwa wagonjwa 50. Upasuaji wa kufungua kifua utafanyika zaidi kwa watoto na watu wazima watafanyiwa zaidi upasuaji wa bila kufungua kifua.
Kwa nama ya kipekee tunaishukuru sana Serikali kupitia Balozi wetu wa nchini Saudi Arabia Mhe. Hemedi Mgaza kwa kutoa kibali cha kuingia nchini (Visa) bila malipo kwa wataalamu wetu hawa ambao wamekuja nchini kutoa matibabu ya moyo bure kwa wagonjwa wetu.
Kama mnavyofahamu matibabu ya moyo ni ya gharama hivyo basi tunaendelea kuwahimiza wananchi  kujiunga na mfuko wa taifa wa bima ya afya ambao utawasaidia kulipa gharama za matibabu pindi  watakapougua na kuhitaji kupata matibabu.

No comments:

Post a Comment