TANGAZO


Monday, February 20, 2017

ZAIDI YA WANANCHI 500 WAPIMA AFYA BONANZA LA WANAHABARI

Maafisa Mawasiliano Serikalini (TAGCO), Viongozi wa Taasisi mbalimbali, Wahariri wa Vyombo vya Habari, Madaktari, Waandishi wa Habari pamoja na Wapiga picha wakifanya mazoezi ya viungo ikiwa ni sehemu ya kulinda miili yao dhidi ya magonjwa yasiyoambukiza pamoja na utekelezaji wa agizo la Mhe. Makamu wa Rais wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan alilolitoa 17 Desemba, 2016 ambalo linawataka Watumishi wa Uma kazini kujenga utamaduni wa kufanya mazoezi. Mazoezi hayo yalifanyika 18/02/2017 katika Viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam. (Picha na Benedict Liwenga-WHUSM)

Na Hassan Silayo
ZAIDI ya wananchi 500 wakiwemo waandishi wa Habari na Maafisa Mawasiliano Serikalini wamepima afya katika bonanza lililoandaliwa na Chama cha Maafisa Mawasiliano Serikalini, Jukwaa la Wahariri na Klabu ya Waandishi Dar es Salaam.

Bonanza hilo lililohusisha pia uchangiaji damu kwa hiari na ufanyaji mazoezi ya viungo ili kuunga mkono agizo la Makamu wa Rais Makamu wa Rais, Mhe. Samia Suluhu Hassan ili kujikinga na magonjwa yasiyoambukiza.

Akiongea mara baada ya kupima afya Sharifa Hussein mkazi wa Ilala Jijini Dar es Salaam amesema kuwa anawapongeza waliofanya uratibu wa kupeleka madaktari kwani imewapa fursa ya kujua hali za afya yao pamoja na kupata ushauri wa kitabibu.

"Niliona tangazo kuhusu upimaji afya hapa, nimekuja nimepima nimepata majibu pamoja na ushauri, kwakweli nawashukuru waandaaji wa shughuli hii, imesaidia wengi kujua hali za afya zao na sasa ni jukumu letu kwenda kufanyia kazi yale tuliyoambiwa baada ya matiWatoto
Alisema Bi.Sharifa.

Akiongea baada ya kumaliza programu ya mazoezi katika viwanja vya Mnazi Mmoja, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Dkt. Ayoub Rioba amesema kuwa watanzania hawana budi kufanya mazoezi mara kwa mara kwani inasaidia kupunguza gharama zinazoweza kutumika kutibu magonjwa yanayoweza kusababishwa na kutofanya mazoezi ambayo yamekuwa yakisumbua wengi hasa gharama za matibabu yake.

Naye Mwenyekiti wa Chama cha Maafisa Mawasiliano Serikalini (TAGCO) Bw. Innocent Mungy amesema kuwa wameamua kuandaa bonanza hilo ili kuunga mkono agizo la makamu wa rais makamu wa Rais Mh. Samia Suluhu Hassan la kufanya mazoezi ili kujikinga na magonjwa yasiyoambuka.

Mwenyekiti wa Jukwaa la wahariri (TEF) Teophil Makunga aliwasisitiza wanannchi kuweka programu binafsi za kufanya mazoezi kwani mazoezi yana saidia kupunguza uwezekano wa kupata magonjwa mara kwa mara pia yanasadia kufikiri na kufanya mambo vizuri.

Mratibu wa Magonjwa Yasiyoambukizwa Dkt Digna Siriwa Alisema kuwa kutokana na ripoti iliyotolewa na Shirika la Afya Duniani (WHO) alisema kuwa  kwa mwaka 2008 asilimia 63 ya watu ulimwenguni walikufa kwa mgonjwa yasiyoambukizwa ikiwemo Presha, Sukari, Kansa pamoja na magonjwa ya mfuko wa hewa ambayo yanaweza kuzuiwa kwa kufanya mazoezi. 

Bonanza hilo limeandaliwa na Chama cha Maafisa Mawasiliano Serikalini, Jukwaa la Wahariri, Klabu ya Waandishi wa habari wa Dar es salaam pamoja na kuratibiwa na Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto.

No comments:

Post a Comment