TANGAZO


Monday, May 9, 2016

WANANCHI WASHAURIWA KUTUMIA HUDUMA ZA MSAADA WA KISHERIA

Wakili wa Serikali Mkuu kutoka Wizara ya Katiba na Sheria Bw. Charles Mmbando akiwaeleza waaandishi wa Habari (Hawapo pichani) kuhusu huduma za msaada wa kisheria kwa wananchi ambao ni wahitaji wa msaada hiyo juu ya masuala mbalimbali yanayowakabili. Kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa wizara hiyo, Bi. Sheiba Bulu. (Picha zote na Hassan Silayo-Maelezo) 
Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia Mkutano huo.

Na Beatrice Lyimo- Maelezo
09/05/2016
Dar es Salaam
SERIKALI imewataka wananchi wasio na uwezo wa kuweka Mawakili au kulipa huduma za kisheria kutumia Mpango wa Huduma za Msaada wa Kisheria kupitia Sekretarieti ya Msaada wa Kisheria na Mashirika yaliyosajiliwa kwa ajili hiyo.

Wito huo umetolewa leo jijini Dar es Salaam na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini  kutoka  Wizaraya Katiba na Sheria  Bi. Sheiba Bulu alipokuwa akiongea na waandishi wa habari kuhusu huduma hiyo inayotolewa na Sekretarieti ya Msaada wa Kisheria na Mashirika yaliyosajiliwa kwa ajili hiyo.

Amesema kuwa lengo kuu la huduma hiyo ni kuhahikisha kila mwananchi anapata haki katika mamlaka husika za utoaji haki na kwa wakati.

“Sekretarieti ya Msaada wa Kisheria inatoa huduma za msaada wa kisheria kwa wananchi ambao ni wahitaji wa msaada wa huduma za kisheria na kuwapa ushauri juu ya masuala mbalimbali yanayowakabili,” aliongeza Bi. Sheiba.

Aidha, kwa upande wake Wakili wa Serikali Mkuu kutoka Wizara hiyo, Charles Mmbando amezitaka asasi na mashirika yanayojishughulisha na huduma ya msaada wa kisheria kwa wananchi kujitangaza  ili kuzidi kutambulika katika jamii  kwani wizara  yake inatambua na kuthamini mchango unaotolewa na mashirika hayo.

Mpango huo ulianzishwa mwaka 2012 ili kuwezesha asasi na Mashirika yasiyokuwa ya kiserikali kupanua wigo wa huduma ya msaada wa kisheria kwa wananchi waishio kwenye maeneo ambayo hawawezi kulipia gharama za mawakili nchini.

No comments:

Post a Comment