TANGAZO


Wednesday, May 25, 2016

KAMPUNI YA STA TRAVEL YAENDELEA KUWA SULUHISHO LA USAFIRI KWA WATANZANIA WANAOSOMA NJE YA NCHI

Mwanafunzi akiwa darasani

Na Frank Shija, MAELEZO
Wanafunzi na vijana wakitanzania kuendelea kunufaida na usafiri wa njia ya anga kwa gharama nafuu kupitia Kampuni ya Sta Travel yenye maskami yake mtaa wa mtendeni manispa ya Ilala jijini Dar es Salaam.

Hayo yamebainishwa na Meneja uendeshajji wa Kampuni hiyo Abass Takim alipokuwa akizungumza na mwandishi wa habari hii ofisini kwake jana.

Takim amesema kuwa watanzania wanaosoma elimu ya juu nje ya nchi wanayofurusa ya kunufaiki na huduma zaokwa kuwaunganisha na usafiri wa gharama ndogo zenye punguzo maalum za kusafiri wakati wa kwenda na kurudi kutoka masomoni katika nchi wanazosomea.

Takkim amesema kuwa taasisi yao imekuwa msaada mkubwa kwa Watanzania wanaopata fursa ya kusoma nje ya nchi kwani wanatoa huduma ya usafiri ikiwa na punguzo maalum la gharama za usafiri ili waweze kumudu gharama hizo, ambapo huduma hiyo ya usafirishaji wa wanafunzi kwa gharama nafuu inaenda sambamba na huduma za malazi kwa gharama nafuu wakati wa kwenda na kurudi,Bima ya safari na  Kitambulisho cha Kimataifa cha Mwanafunzi

Aliongeza kuwa mpaka sasa Taasisi yake imetoa huduma ya hiyo kwa watanzania wengi hasa wanafunzi wanaoenda kusoma katika vyuo vya Kuala Lumpar Malyasia, London Uingereza, na Guangzhou China.

Aidha Abbas alisema kuwa pamoja na kutoa huduma hiyo kwa watanzania kumekuwa na changamoto katika upatikanajji wa Viza kwa wateja wao na kupelekea kujitokeza kwa usumbufu, hata hivyo Sta Travel imekuwa ikijitahidi kuwasaidia wateja wake ili wakamilishe taratibu zao kwa wakati.

Sta Travel niasasi inayojihusisha na utoaji wa huduma ya kusafirisha wanafunzi kwa gharama nafuu ikiwa na punguzo kwa lengo la kuwasaidia watanzania kufikia ndoto zao bila kuwapo na kikwazo.


Katika kuhakikisha inafikia wateja wake kwa urahisi zaidi Sta Travel imefungua zaidi ya matawi 400 katika nchi 100 dunia kote ambapo kwa Tanzania ofisi zake zinapatikana katika mtaa wa Mtendeni, Kisutu (Posta),Takims Holidays / STA Travel Partner mkabala na Supermarket ya Shrijee jijini Dar es Salaam unaweza pia kuwasiliana nao kupitia simu namba +255 758 828384/85 au tembelea tovuti yao http://www.escape-tanzania.com/

No comments:

Post a Comment