TANGAZO


Friday, February 12, 2016

Naibu waziri Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo atoa pongezi kwa Twiga Stars

Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia James Wambura (katikati) akipokelewa na Katibu Mkuu Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Bw. Mwesigwa Celestine (kulia) alipofanya ziara katika katika ofisi za TFF na kuzungumza na wachezaji wa timu ya taifa ya mpira wa miguu ya wanawake (Twiga Stars) leo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Maendeleo ya Michezo Bw. Makoye Nkenyenge. 
Katibu Mkuu Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Bw. Mwesigwa Celestine (kulia) akimuonyesha Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia James Wambura (wapili kulia) moja ya ofisi zinazotumiwa na TFF wakati Mhe. Waziri alipofanya ziara katika katika ofisi hizo leo Jijini Dar es Salaam. Wapili kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Maendeleo ya Michezo Bw. Makoye Nkenyenge.
Katibu Mkuu Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Bw. Mwesigwa Celestine (aliyesimama) akizungumza na ugeni ulioongozwa naNaibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kutembelea ofisi za TFF pamoja na kuzungumza na wachezaji wa Twiga Stars leo Jijini Dar es Salaam. Watatu kulia ni Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia James Wambura, kulia ni Kaimu Mkurugenzi Idara ya Michezo Bw. Makoye Nkenyenge. 
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia James Wambura akizungumza na wachezaji wa Twiga Stars (hawapo pichani) leo jijini Dar es Salaam baada ya kutembelea ofisi za TFF na kukutana na wachezaji hao kuwahamasisha wazidi kufanya vizuri katika mashindano mbalimbali ndani na nje ya nchi. Kushoto ni Katibu Mkuu Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Bw. Mwesigwa Celestine. 
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia James Wambura (wanne kushoto) katika picha ya pamoja na viongozi na wachezaji wa Twiga Stars leo jijini Dar es Salaam baada ya kufanya ziara katika ofisi za TFF na kuzungumza na wachezaji hao kuwahamasisha wazidi kufanya vizuri katika mashindano mbalimbali ndani na nje ya nchi. Watatu kushoto ni Katibu Mkuu Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Bw. Mwesigwa Celestine na wanne kulia ni mwenyekiti wa chama cha mpira wanawake Bibi. Amina Karuma. 
Wafanyakazi wa TFF katika picha ya pamoja na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia James Wambura (wanne kushoto) alipotembelea ofisi za TFF leo jijini Dar es Salaam. Wapili kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Maendeleo ya Michezo Bw. Makoye Nkenyenge na wapili kulia ni Katibu Mtendaji Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Bw. Henry Lihaya. (Picha zote na Genofeva Matemu - Maelezo)

No comments:

Post a Comment