TANGAZO

Tuesday, November 24, 2015

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Majaliwa atembelea Tamisemi

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Majaliwa Kassim Majaliwa akiongea na baadhi ya vingozi na watendaji wakuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) alipotembelea Wizara hiyo kwa lengo la kuongea viongozi hao kuhusu utendaji kazi wenye tija kwa wananchi leo jijini Dar es Salaam. 

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Majaliwa Kassim Majaliwa (kushoto aliyevaa tai nyekundu) akisalimiana na viongozi mbalimbali wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) mara baada ya kuwasili Wizarani hapo kwa ziara fupi leo jijini Dar es Salaam. 

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Jumanne Sagini, akitoa taarifa fupi kwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Majaliwa Kassim Majaliwa alipotembelea Wizara hiyo leo jijini Dar es Salaam. 
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) anayeshughulikia Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Kabyamukama Kiliba akitoa neno la shukrani mara baada ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Majaliwa Kassim Majaliwa kumaliza kuongea na viongozi wa TAMISEMI leo jijini Dar es Salaam. 
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Majaliwa Kassim Majaliwa (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Jumanne Sagini (wa pili kushoto) pamoja na Manaibu Katibu Wakuu wa Wizara hiyo. 
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Majaliwa Kassim Majaliwa (katikati walioketi) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa Wizara ya TAMISEMI leo jijini Dar es Salaam. 

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Majaliwa Kassim Majaliwa akiagana na baadhi ya viongozi mara baada ya kumaliza ziara yake TAMISEMI leo jijini Dar es salaam. (Picha zote na Mangi-Maelezo)

NA Eleuteri Mangi-Maelezo
WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Majaliwa Kassimu Majaliwa amewataka Watendaji wakuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) kutekeleza majukumu yao kwa weledi kwa kuzingatia taaluma zao ili kufikia malengo waliyojiwekea.

Waziri Mkuu Majaliwa alisema hayo leo jijini Dar es salaam alipokuwa akiongea na viongozi wa wizara hiyo katika ziara yake ya kujitambulisha, kufahamiana na kupeana kazi.

“Kipindi hiki ni kipindi cha uwajibikaji, natamani katika kipindi kifupi kuwe na mabadiliko katika sekta zote zinazosimamiwa na TAMISEMI” alisema Waziri Mkuu Majaliwa.
Akiongea na viongozi wa wizara  hiyo Waziri Mkuu Majaliwa alisisistiza kuwa kila mmoja ajitume kwa kuzingatia mambo muhimu ya kazi ikiwemo kuwahi kazini, kuzingatia utendaji kazi unaozingatia sheria, kanuni na taratibu za utumishi wa umma ili kufikia malengo na mipango ya kazi yenye tija kwa taifa na kwa manufaa ya wananchi.

Ili kuwa na ufanisi katika kazi katika Serikali ya Awamu ya Tano, Waziri Mkuu Majaliwa aliongeza kuwa kila Mkuu wa Idara, Vitengo na Taasisi awe na hotuba ya Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli ambayo ndiyo dira ya Serikali yake.

Aidha, Waziri Mkuu Majaliwa alisema kuwa TAMISEMI ni injini ya maendeleo kwa wananchi, hivyo ni wajibu wa viongozi na watumishi kuongeza, kuimarisha uadilifu na uaminifu katika utumishi wa umma na kuwaasa viongozi hao kukemea wizi, uzembe na ubadhirifu katika maeneo yao ya kazi.

Akizungumza kwa niaba ya wafanyakazi wa (TAMISEMI), Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Bw. Jumanne Sagini amesema kuwa watumishi katika wizara hiyo wanawajibu wa kufanya kazi kwa bidii kwa kuzingatia maadili ya kazi pamoja na kujiepusha na tabia zisizoendana na utumishi wa umma.

Vile vile Katibu Mkuu Sagini amemhakikishia Waziri Mkuu kuwa ofisi ya TAMISEMI itafanya naye kazi kwa kasi kubwa kwa kuzingatia sheria na kanuni zilizopo katika ofisi hiyo ili kuleta mafanikio chanya ndani ya Serikali kwakuwa ofisi hiyo ndiyo inayoshughulikia kwa kiasi kikubwa utekelezaji wa sera za maendeleo kwa wananchi.

Hata hivyo Katibu Mkuu Sagini ameziagiza halmashauri zote nchini kuhakikisha zinasimamia ujenzi wa nyumba za waalimu,madarasa pamoja na maabara kwakuwa wao ndio wenye mamlaka ya kusimamia suala hilo katika utekelezaji wake.

Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikal za Mitaa ina idara 11, vitengo sita, na taasisi tano zenye jumla ya watumishi 473 kati yao wanaume 255 na wanawake 218, pamoja na ofisi ndogoDar es salaamyenye jumla ya watumishi 30 kati yao wanaume 16 na wanawake 14.

No comments:

Post a Comment