TANGAZO


Monday, August 3, 2015

Spunda achukua fomu ya kuwania nafasi ya Urais

Ofisa wa NEC, Adam Nyando (kushoto) akimkabidhi 
fomu ya urais, Hashim Rungwe. (Picha zote kwa hisani ya Gloal Pablishers)

Ofisa wa NEC, Crecencia Mayalla (kushoto),akimpatia
maelekezo mgombea namna ya kujisajili katika daftari la wagombea.
Hashim Rungwe (kushoto) akiwa na mgombea 
mwenza, Isa Abbas Husein (kulia), wakati akipewa
maelekezo ndani ya ofisi hizo.

Mgombea urais, Hashim Rungwe kupitia Chama cha 
Ukombozi wa Umma (Chaumma) akiwaonyesha 
wanahabari (hawapo pichani) mkoba ulio na fomu 
ya kugombea urais.
Hashim Rungwe (kulia) akiwa na mgombea mwenza,
Isa Abbas Husein (kushoto), wakitoka ndani ya Ofisi
za Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).

Wanahabari wakiwa nje ya ofisi za NEC wakimsubiri
mgombea urais wa Chaumma.
                              
Na Anitha Jonas
MGOMBEA wa nafasi ya Urais kupitia Chama 
cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA), Bw. 
Hashim Rungwe Spunda amechukua fomu 
rasmi katika ofisi za Tume ya Uchaguzi ya Taifa
nchini.

Akikabidhiwa fomu hiyo na mmoja wa Afisa wa Tume 
hiyo Bw. Adam Nyando leo jijini Dar es Salaam Bw. 
Spunda alisema lengo lake la kugombea nafasi hiyo 
ni kuwasaidia Watanzania na kuwatumikia kwa  
uadilifu.

“Nafasi hii ni ya juu sana katika uongozi na inahitaji
uwajibikaji na siyo kuweka tamaa za kujineemesha
huku ukiwaacha wananchi ambao ndiyo walipa kodi 
katika mazingira magumu na bila maendeleo, pia 
nafasi hii siyo ya kulilia kuipata kwa nguvu,”alisema 
Bw. Spunda.

Aidha, mgombea huyo aliipongeza Tume ya Uchaguzi kwa kuliendesha zoezi la uchukuaji fomu vizuri bila tatizo lolote pia ametoa wito kwa wagombea wengine watakaokwenda kuchukua fomu wazingatie masharti yaliyowekwa kwa ikiwemo wasindikizaji wachache na utulivu.

Mbali na hayo Bw.Spunda alishagombea nafasi hiyo 
ya Urais katika uchaguzi wa mwaka 2010 kupitia 
chama cha NCCR-Mageuzi na kushinda kwa asilimia 


moja (1%).

No comments:

Post a Comment