TANGAZO


Monday, August 31, 2015

Global Peace Foundation tawi la Tanzania kuhamasisha amani kuelekea uchaguzi mkuu

Viongozi mbalimbali wakiwa katika uzinduzi huo.
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Global Peace Foundation Tawi la Tanzania (GPFTZ), Martha Nghambi (katikati), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam jana  
wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kuhamasisha amani nchini Tanzania katka kipindi hiki  kuelekea uchaguzi mkuu. Kulia ni Mkurugenzi wa Baraza la Taasisi ya Viongozi wa Dini Tanzania (IRCPT), Mchungaji Thomas Goda na kushoto ni Ofisa Utawala wa GPFTZ, Hilda Ngaja.
Mkurugenzi wa Baraza la Taasisi ya Viongozi wa Dini Tanzania (IRCPT), Mchungaji Thomas Goda (kushoto), akizungumza katika mkutano huo. Kulia ni Balozi wa Amani wa GPF, Dk.Ulimwengu.
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Global Peace Foundation Tawi la Tanzania (GPFTZ), Martha Nghambi (kushoto) na  Mkurugenzi wa Baraza la Taasisi ya Viongozi wa Dini Tanzania (IRCPT), Mchungaji Thomas Goda, wakionesha kipeperushi kinacho hamasisha kushiriki uchaguzi kwa amani.
Ofisa Utawala wa Shirika hilo, Hilda Ngaja (kushoto) na Balozi wa Amani wa GPF, Dk.Ulimwengu (kulia), wakionesha kipeperushi kinacho hamasisha kushiriki uchaguzi kwa amani.
Mkutano na wanahabari ukiendelea.
Wanahabari kutoka vyombo mbalimbali wakichukua taarifa hiyo.

Na Dotto Mwaibale
GLOBAL  Peace  Foundation Tawi  la  Tanzania (GPFTZ), kwa kushirikiana  na    Mshirika  wake, Baraza  la  Wadhamini  la  Taasisi  ya  Viongozi wa  Dini  Tanzania (IRCPT),  wamezindua kampeni  ya  kuhamasisha  Amani  nchini Tanzania  katika  kipindi  hiki  kuelekea uchaguzi  mkuu ,  jina  la  kampeni  ni  “Amani Kwanza”.  

Lengo  kuu  la    kampeni hiyo  ni  kuhamasisha  watanzania  wote  kushiriki    katika  Uchaguzi  Mkuu  kwa  Amani  ambao  unatarajia  kufanyika  siku  ya  25/08/2015.

Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa kampeni hiyo Dar es Salaam leo asubuhi, Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Global Peace Foundation Tawi la Tanzania (GPFTZ), Martha Nghambi  alisema.

Walengwa  wakuu  wa  Kampeni  hiyo  ni  Wanawake na  Vijana ambao  ni  wengi  zaidi  ukilinganisha  na rika  na  makundi  mengine,  na  pia  Wanawake wamekuwa  wakihathirika zaidi  endapo  inapotokea machafuko  hali kadhalika  Vijana  wamekuwa chanzo        cha  uchochezi  wa  machafuko  katika nchi  mbalimbali  duniani.
·  
Kampeni hii  haina  lengo  lolote  la  kuunga  mkono   ama  kupinga  Chama  chochote  cha  Kisiasa  au mgombea  wake,  na  wala  haina  mahusiano yoyote ya  kisiasa na kauli kauli  mbiu  yake ni  “KURA YANGU  UZALENDO  WANGU,  AMANI  YA NCHI YANGU  NI  JUKUMU  LANGU” alisema Nghambi.

Nghambi alisema Kampeni hiyo  imeandaliwa maalumu  kwa  malengo  ya kuwahamasisha Wanawake  na  Vijana  kuwa  mabalozi  wazuri  wa   kulinda  na  kuitetea  Amani  ya  nchi  yetu  hasa katika  kipindi  hiki  kuelekea  uchaguzi Kujiepusha na  vitendo  mbalimbali    ambavyo  vinaweza kuchochea  uharibifu  wa  Amani  nchini Kuhamasisha kila  mmoja  ashiriki  uchaguzi  kwa  amani Ili kuhakikisha.  

Alisema kampeni hiyo inafanikiwa  kutokana na Shirika  la Global  Peace kushirikiana kwa  karibu  na vyombo  vya  habari  nchini  vikiwemo  Radio, Luninga,  Magazeti,  na  mitandao  mbalimbali    ya Kijamii  ikiwemo Twitter,  Face  Book,  instagram  na YouTube.  

Alisema  shirika hilo ni Tawi  la  Taasisi  ya  Kimataifa isiyo ya  Kiserikali  na  isiyotengeneza  faida  Global Peace  Foundation  (GPF)  yenye  makao  makuu yake    Washington  DC,  nchini  Marekani.    

Alisema  shirika  hilo linahamasisha  kutetea  na kulinda  Amani  dunia  ,    shirika  hili  linaamini  ya kuwa “ Kwa  Mungu  sisi  wote  ni  familia  moja” GPF inafanya  kazi  kwa  karibu  na  mitandao  ya kiserikali  na  watu  binafsi  katika  kuendeleza  jamii, Taifa  na  katika  kujenga  na  kulinda  misingi  na maadili  katika  jamii  husika.

GPF  ina  rekodi  nzuri  ya  kufanya  kazi  kwa  karibu na  kwa  mafanikio  makubwa    kuhamasisha  na kulinda  Amani  katika  nchi  mbalimbali  dunia katika bara  la  Afrika,  Asia,  Ulaya  na  Amerika.

Kwa  upande  wa  Afrika,  shirika  hili  limekuwa likijihusisha  na  maswala  mbalimbali  ya  kijamii katika  nchi  za  Kenya,  Uganda  na  Nigeria kudumisha  Amani  kwenye  ukanda  wa  Afrika.
(Imeandaliwa na Dotto Mwaibale)

No comments:

Post a Comment