TANGAZO


Sunday, July 5, 2015

Wikileaks:Marekani iliichunguza Brazil

Dilma Rousseff
Mtandao wa Wikileaks umesema kuwa una ushahidi kwamba baadhi ya maafisa wakuu wa taifa la Brazil walipelelezwa mara kadhaa na idara ya ujasusi nchini Marekani NSA.
Habari hizo zinasema kuwa Idara hiyo hususan ilipeleleza uchumi wa taifa hilo.
Wikileaks ilichapisha orodha ya nambari 29 za simu za raia wa Brazil waliopo katika sekta za benki,fedha na uchumi.
Kulingana na mtandao huo udukuzi huo ulianza mapema mwaka 2011 na huenda hata mapema zaidi.
Rais Dilma Rousseff alikatiza ziara yake mjini Washington miaka miwili iliopita baada ya aliyekuwa mchambuzi wa maswala ya ujasusi Edward Snowden kufichua kwamba simu zake pamoja na barua pepe zilikuwa zikichunguzwa.
Uchapishaji huo ulibaini kwamba upelelezi huo haukumlenga rais Dilma Rousseff pekee bali pia katibu wake,pamoja na afisa mkuu wa idara ya wafanyikazi aliyekuwa waziri wa fedha Antonio Palocci.
Afisi yake ya nyumbani na hata simu zake katika ndege yake zilichunguzwa kwa mujibu wa Wikileaks.

No comments:

Post a Comment