TANGAZO


Friday, March 27, 2015

Zuwena, Msusi aliyejishindia shilingi milioni 10

*Akabidhiwa kitita chake Tabata Segerea 
Milionea kupitia Promosheni ya Jaymillions inayoendeshwa na Vodacom Tanzania, Ibrahim Ibrahim (kushoto) akimkabidhi hundi yenye thamani ya shilingi Milioni 10/- Zuwena Rajabu (kulia), aliyeibuka mshindi wa kitita hicho kupitia Promosheni hiyo wiki hii. Anayeshuhudia katikati ni Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Matina Nkurlu. Hafla hiyo ilifanyika Tabata Segerea  jijini Dar es Salaam, Ili  mteja kujua kama  ameshinda anatakiwa kutuma neno JAY au AUTO kwenda namba 15544.
Mshindi wa  Promosheni ya Jaymillions inayoendeshwa na Vodacom Tanzania, Zuwena Rajabu (kulia), akisoma hundi yake yenye thamani ya shilingi Milioni 10/- wakati wa hafla fupi ya kukabidhiwa hundi hiyo na Milionea mwenzake Ibrahim M. Ibrahim (kushoto) na Meneja Uhusiano wa kampuni hiyo Matina Nkurlu(katikati).Hafla hiyo ilifanyika Tabata Segerea  jijini Dar es Salaam. Ili mteja kujua kama ameshinda anatakiwa kutuma neno JAY au AUTO kwenda namba 15544.
Milionea kupitia Promosheni ya Jaymillions inayoendeshwa na Vodacom Tanzania, Ibrahim Ibrahim (kushoto) na Meneja wa kampuni hiyo Matina Nkurlu (katikati) wakimpongeza Mshindi wa  Promosheni ya Jaymillions, Zuwena Rajabu baada ya kumkabidhi hundi yake yenye  thamani ya kitita cha shilingi Milioni 10/- alizojishindia kupitia promosheni hiyo. Hafla ya makabidhiano hayo ilifanyika Tabata Segerea  jijini Dar es Salaam. Ili mteja kujua kama ameshinda anatakiwa kutuma neno JAY au AUTO kwenda namba 15544.
Zuwena Rajabu ambaye ni Mshindi  kupitia  Promosheni ya Jaymillions inayoendeshwa na Vodacom Tanzania, akiongea na waandishi wa habari baada ya kukabidhiwa  hundi yake yenye thamani ya shilingi Milioni 10/- wakati wa hafla fupi iliyofanyika Tabata Segerea  jijini Dar es Salaam ya kukabidhiwa hundi hiyo na Milionea mwenzake Ibrahim M. Ibrahim na Meneja Uhusiano wa kampuni hiyo Matina Nkurlu (hawapo pichani). Ili mteja kujua kama ameshinda anatakiwa kutuma neno JAY au AUTO kwenda namba 15544.
Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Matina Nkurlu (katikati), akimsomea hundi yake Zuwena Rajabu (kulia) wakati wa hafla fupi ya kumkabidhi hundi hiyo yenye thamani ya kitita cha shilingi milioni 10/- alizojishindia kupitia promosheni ya JayMillions inayoendeshwa na kampuni hiyo hivi karibuni. Anayeshuhudia kushoto ni Milionea kupitia Promosheni hiyo Ibrahim M. Ibrahim. Hafla hiyo ilifanyika Tabata Segerea jijini Dar es Salaam. Ili mteja kujua kama ameshinda anatakiwa kutuma neno JAY au AUTO kwenda namba 15544.

Na Mwandishi wetu
BINTI msusi anayefanya kazi ya ususi na mkazi wa Tabata Segerea Zuwena Rajabu (22) leo amekabidhiwa kitita cha shilingi milioni 10/-alizojishindia kupitia promosheni ya Jaymillions inayoendeshwa ka Vodacom Tanzania.
Zuwena alikabidhiwa fedha zake na milionea mwenzake aliyemtangulia Ibrahim M. Ibrahim,Ambaye ni mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha St.Joseph yeye alikabidhiwa kitita chake cha milioni 10 wiki iliyopita.Makabidhiaano hayo yalifanyika katika saluni anapofanyia kazi Zuwena iliyopo Tabata Segerea mbele ya wafanyakazi wenzake na waandishi wa habari.

Akiongea muda mfupi baada ya kupokea fedha zake za ushindi,Zuwena alisema anamshukuru Mwenyezi Mungu amemuona na ameweza kusikia maombi yake ya kupata mtaji wa kuanzisha saluni yake ya kike ya kisasa na duka la kuuza Vipodozi imetimia.
“Naishukuru sana Vodacom Tanzania wamefanya ndoto yangu ya kuwa mfanyabiashara mkubwa kutimia na huu ni uthibitisho kuwa   promosheni ya Jaymillions imelenga kuwakomboa wanyonge kutoka hali ya chini na kuwapandisha kwenda hali ya juu”.Alisema Zuwena kwa furaha.

Promosheni ya Jaymillions iliyoanza katikati ya mwei Januari mwaka huu ambayo itadumu kwa muda wa siku 100 imeleta faraja na itaendelea kuleta faraja na mafanikio kwa wateja wa kampuni hiyo kwa kuweza kujinasua katika hali duni ya maisha na maisha kuwa murua na hadi kufikia sasa amekwishapatikana mshindi mmoja wa milioni 100/-,washindi wanne wa milioni 10/-na washindi 38 wa milioni 1/-.
Mshindi wa milioni 100/-ni Uwezo Madengenya kutoka wilayani Kilolo mkoani Iringa.Washindi wa milioni 10/-mbali na Zuena aliyekabidhiwa kitita chake leo ni Hyness Petro  Kanumba kutoka Rukwa,James Mangu (Mwanza), na Deborah Stanley ambaye naye ni anafanya kazi ya ususi na mkazi wa Kimara kwa Komba jijini Dar es Salaam.

Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania Matina Nkurlu,akiongea katika hafla hiyo alimpongeza mshindi huyo na kusema kwamba fedha hizo zimeenda kwa mshindi sahihi kwani mshindi huyu ana malengo mazuri ya matumizi ya fedha zake kwa kujiendeleza kibiashara.

Pia aliwahimiza wateja wote kuchangamkia promosheni  ya Jaymillions katika kipindi hiki ambacho inakaribia kufika mwishoni ili wajishindie kwa kuhakikisha wanatuma neno JAY kwenda namba 15544ili kutopoteza bahati zao za kushinda.Aliitaja njia nyingine ya kushinda kuwa ni kutuma neno AUTO kwenda namba 15544 iwapo simu haina fedha ambapo mteja akiweka fedha anakatwa shilingi 300/-tu.

No comments:

Post a Comment