TANGAZO


Friday, March 27, 2015

Tanzania yachaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Mawaziri wa Fedha, Uchumi na Mipango ya nchi wanachama wa Umoja wa Afrika (AU) na Kamisheni ya Uchumi ya Afrika (ECA)

Viongozi wakiwa kwenye meza kuu katika kikao cha Kamati ya watalaam wa Fedha, Uchumi na Mipango kinachoendelea Mjini Addis Ababa –Ethiopia
Na Idara ya Habari, Maelezo
TANZANIA imechaguliwa kuwa Mwenyekiti wa kamati ya Watalaam wa Fedha, Uchumi na Mipango kwa nchi wanachama wa Umoja wa Afrika (AU) na Kamisheni ya Uchumi ya Afrika (ECA) kwa kipindi cha mwaka mmoja.

Uchaguzi huo ulifanyika baada ya ufunguzi wa kikao cha Kamati ya watalaam wa Fedha, Uchumi na Mipango ambacho kinaendelea Mjini Addis Ababa –Ethiopia. Kabla ya uteuzi huo nafasi hiyo ya Mwenyekiti ilikuwa inashikiliwa na Nigeria.

Ukanda wa nchi za Mashariki mwa Afrika ulipewa nafasi ya kuwa mwenyekiti na wajumbe wa nchi kutoka ukanda huo kwa pamoja waliichagua  wajumbe hao waliipa Tanzania heshima hiyo. Nchi zilizoipigia kura Tanzania kuwa Mwenyekiti  ni Ethiopia, Eritrea, Madagascar, Kenya, Uganda, Burundi, Rwanda,Sudan Kusini, Djibout, Somalia, Msumbiji, Comoro, Mauritius na Seychelles.

Pamoja na Tanzania kuwa Mwenyekiti wa Mkutano huo, pia Misri ilichaguliwa kuwa Makamu wa kwanza wa Mwenyekiti ikiwakilisha nchi za Kaskazini mwa Afrika,Gabon kuwa Makamu wa pili wa Mwenyekiti ikiwakilisha nchi za Afrika ya kati,Afrika ya Kusini Makamu wa tatu wa Mwenyekiti ikiwakilisha nchi za Kusini mwa Afrika na Guinea ilichaguliwa kuwa Katibu ikiwakilisha nchi za Afrika Magharibi.

No comments:

Post a Comment