TANGAZO


Monday, January 26, 2015

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idd ahudhuria hafla ya kuapishwa Rais wa Zambia

Mtoto wa Kizambia Anna Samwel Munata akimkabidhi ua Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi ikiwa ishara ya makaribisho kwenye uwanja wa ndege wa  Kimataifa wa Keneth Kaunda alipohudhuria kuapishwa kwa Rais Mpya wa Nchi hiyo Bwana Edgar Chagwa Lungu. Kulia ni Waziri wa Kazi na huduma za Kijamii wa Serikali ya Jamuhuri ya Zambia Bwana  Fackson Shamenda. 
Balozi Seif akisalimiana na Maafisa wa Ubalozi wa Tanzania waliopo Lusaka Zanzbia kwenye uwanja wa ndege wa Keneth Kaunda akishindikizwa na Balozi wa Tanzania Nchini Zambia Balozi Grace Mujuma, Waziri wa Kazi ya Huduma za Kijamii wa Zambia Bwana Fackson Shamenda pamoja na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania Mh. Mahadhi Juma Maalim.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akiwa pamoja na Balozi wa Tanzania Nchini Zambia Balozi Grace Mujuma kushoto yake na Waziri wa Kazi ya Huduma za Kijamii wa Zambia Bwana Fackson Shamenda kulia yake wakielekea mapokezi mara baada ya kuwasili uwanja wa ndege wa Keneth Kaunda.
Balozi Seif akiwa pamoja na Viongozi wake wa Kimataifa wakishuhudia uapishwaji wa Rais Mpya wa Zambia Bwana Edgar Chagwa Lungu kwenye uwanja wa Michezo wa Mshujaa Mjini Lusaka Nchini Zambia. 
Rais wa Zimbabwe ambae pia ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Nchi za Kusini na Mashariki mwa Afrika (SADC), Dk. Robert Gabriel Mugabe Kushoto akiwa na Rais Mstaafu wa Zambia Dr. Keneth Kaunda wakishuhudia uapishwaji wa Rais Mpya wa Zambia Bwana Edgar Chagwa Lungu.
Mwananchi wa Zambia akionyesha furaha na kumuunga mkono Rais mpya wa Nchi hiyo Bwana Edgar Chagwa Lungu wakati wa sherehe za kuapisha kwake katika uwanja wa mashujaa Mjini Lusaka. (Picha zote na – OMPR – ZNZ)

No comments:

Post a Comment