Wahariri wa Vyombo vya Habari nchini wakiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara wakati wa kikao kazi cha Maofisa Mawasiliano Serikalini leo Mjini Mtwara.
Baadhi ya Maafisa Mawasiliano wakiwa
katika picha ya pamoja na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt.
Fenella Mukangara wakati wa kikao kazi cha Maofisa Mawasiliano Serikalini leo
Mjini Mtwara.
Mhadhiri wa Chuo kikuu cha Tiba na
Sayansi Shirikishi(MUHAS) Dkt.Ave Maria Semakafu akiwaeleza jambo Waziri wa
Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara (kushoto), na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bi. Sihaba Nkinga.
Mjumbe
wa Jukwaa la wahariri Bw. Salim Salim akiwaeleza washiriki wa mkutano huo
Umuhimu wa kuwa na Usiri katika utendaji kazi. (Picha zote na Hassan Silayo)
Na
Frank Mvungi-MAELEZO
SERIKALI imevitaka vyombo vya Habari nchini kuwaelimisha wananchi kuhusu Katiba
inayopendekezwa ili waweze kujitokeza kwa wingi kuipigia kura.
Hayo
yamesemwa na Waziri wa Habari Vijana utamaduni na Michezo Mh.Dkt Fenella
Mukangara wakati wa akifungua kikao Kazi cha Maafisa Mawasiliano Serikalini
kinachofanyika Mkoani Mtwara.
Akifafanua
Mh.Dkt Mukangara amewataka Maafisa Mawasiliano Kushirikiana na vyombo vya
habari katika kuuelimisha umma kuhusu Katiba nayopendekezwa ili wananchi waweze
kufanya uamuzi sahihi wakati wa kupiga kura ya maoni.
Akizungumzia
swala la wananchi kujiandisha ili wapate
fursa ya kupiga kura ya maoni Dkt Mukangara amesema ni vyema Maafisa Mawasiliano
wakashirikiana na vyombo vya habari, kuwahamasisha wananchi kujiandisha kwa
wakati muafaka.
Pia
Waziri Mukangara alisisitiza kuwa Serikali kwa kutambua umuhimu wa kuimarisha
uhuru wa wajibu wa vyombo vya habari pamoja na wajibu wa Maofisa Mawasiliano
kutoa taarifa kwa umma ndio maana imeandaa kikao kazi hicho.
Aidha
Dkt. Fenella alisema kuwa ushirikiano kati ya Maafisa Mawasiliano Serikalini na
Wahariri wa vyombo vya habari hapa nchini utasaidia kutafuta namna bora ya
kutoa habari kwa umma na kwa usahihi na weledi unaohitajika.
Kikao
Kazi cha Maafisa Mawasiliano Serikalini kinafanyika Mkoani Mtwara kuanzia
Januari 26,hadi februari Mosi 2015 katika ukumbi wa NAF Hotel Mkoani Mtwara
kikiwashirikisha wahariri wa vyombo kutoka vyombo mbalimbali vya Habari hapa
nchini.
No comments:
Post a Comment