TANGAZO


Monday, December 15, 2014

MATOKEO YA SEHEMU MBALIMBALI YA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA YALIYOTOLEWA


CCM YANYAKUA VITI VYOTE SINGIDA

Na Jumbe Ismailly, Singida
Dec,15,2014      
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) katika Manispaa ya Singida kimeibuka na ushindi katika uchaguzi wa serikali za mitaa uliomalizima juzi baada ya kuzoa nafasi zote 50 za nafasi ya mwenyekiti wa mitaa, ambayo ni sawa na aslimia mia moja.

Msimamizi wa uchaguzi huo wa Manispaa ya Singida,Joseph Mchina aliyasema hayo alipokuwa akitoa taarifa ya matokeo ya uchaguzi huo kwa waandishi wa Habari na kudai kwamba uchaguzi huo umefanyika kwa amani na utulivu.
Alifafanua Mchina ambaye pia ni Mkurugenzi wa Manispaa ya Sin gida kwamba kwa upande wa uchaguzi wa serikali za vijiji,CCM imeshinda katika vijiji 19 dhidi ya 20 vya Manispaa hiyo na kwamba ushindi huo ni wa aslimia 95.
"CUF ilishinda nafasi moja ya Kijiji sawa na asilimia tano, CHADEMA na ACT havikuambulia kitu",alisisitiza Msimamizi huyo.

Aidha Mchina alisema katika vitongoji 90 vilivyopo katika Manispaaya Singida, CCM imenyakua vitongoji 81 sawa na aslimia 90, CUF kimeshinda vitongoji nane sawa na aslimia 8.9 na CHADEMA imeambulia kitongoji kimoja sawa na aslimia 1.1.
Kwa mujibu wa msimamizi huyo alisema CCM imepita bila kupigwa kwenye nafasi za uenyeviti wa vijiji 6 (asilimia 30), Vitongoji 37 (aslimia 41.1), wenyeviti wa mitaa 13 (asilimia 26 na CUF vitongoji 2.

Katika hatua nyingine katika wilaya ya Ikungi,Msimamizi wa uchaguzi huo Mohamedi Nnkya alisema bado wanaendelea kukamilisha kazi ya kuhesabu kura na matokeo kamili,yatatangazwa kesho (leo 16/12/2014).

Hata hivyo habari za uhakika kutoka ndani ya wilaya hiyo yenye majimbo ya Singida mashariki na magharibi,CHADEMA imekisulubu CCM kwa kunyakua karibu nafasi zote zilizokuwa zikigombewa.

Matokeo Kiteto ya uchaguzi
Na Mohamed Hamad Manyara
Matokeo ya awali uchaguzi wa serikali za mitaa yameanza kutolewa na wasimamizi wasaidizi katika kata mbalimbali mkoani Manyara ambapo wilaya ya Kiteto vijiji 26 kati ya 63 ndivyo vilivyoshiriki uchaguzi wa Serikali za mitaa

Kata ya Matui kituo cha Azimio A. Chadema wamepata kura 547 CCM 100, Azimio B Chadema 450 na CCM 324 huku kura sita zikiwa zimeharibika, Namanga Chadema 341 CCM 280, Soweto Chadema 131 na CCM 352, Kivukoni Chadema 255 na CCM 154, Bwawani Chadema 192 na CCM 205, Mjengo Chadema 262 na CCM 272

Kata ya Sunya Juhudi CCM 35 Chadema 178,Ngapune CCM 7 Chadema 126, Kichangani 51 Chadema 178,Mnadani CCM 126 Chadema 91,Mji mpya CCM 86 Chadema 72, Ibutu CCCM 126 Chadema 53, Kiegea CCM 122 Chadema 19, Lendulu CCM 7 Chadema 70

Katika kata ya Lengatei Kijiji cha Zambia kituo cha Ngalanga CCM 84 Chadema 21, Zambia CCM 68 Chadema 48, Stamili CCM 100 Chadema 35 Makanya CCM 61 Chadema 96, Mfunpala CCM 31 Chadema 70
Kata ya Kaloleni CCM 77 Chadema 322, Vumilia NCCR Mageuzi 107 CCM 105, Mtaa msikitini CCM imeshinda kwa kura 6 mtaa wa Shirangaa CCM imeshinda pamoja na mtaa wa Majengo huku kibaya kati nayo ikichukuliwa na CCM

Kwa Wilaya ya Mbulu kulikuwa na vijiji 105 ambapo 95 waliogombea ni CCM na Chadema,1 NCCR Mageuzi na CCM, huku 14 CCM ikipita bila kupigwa na vitongoji vilikuwa 575 huku CCM ikipita bila kupingwa vitongoji 150

Kwa mujibu wa Msimamizi wa Uchaguzi wilaya Bw. Bosco Nduguru amesema kuwa matokeo ya pamoja hayajapatikana kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo umbali wa kutoka eneo moja kwenda jingine

“Wilaya ya Kiteto ina changamoto kubwa zikiwemo umbali kutoka makao makuu ya wilaya na maeneo mengine ambapo kata ya Sunya kuna umbali wa km 120 na uwezekano wa kupata matokeo kwa mara moja unakuwa mgumu”alisema

Hali kadhali katika maeneo ya Simanjiro,Babati mjini na Vijijini,
Mbuli,Hanang ni miongoni mwa maeneo ambayo yanakabiliwa na changamoto za usafiri kufika makao makuu kwa wakati kwaajili ya matokeo hayo
Uchunguzi uliofanywa na Jambo leo umebaini kuwepo kwa changamoto mbalimbali katika zoezi hilo zikiwemo za watu kutojua kusoma na kuandka ambapo hilo liligundulika katika daftari walilojiandikisha wapiga kuwa kuwa wengi wao wamesaini kwa dole gumba.
Hadi saa moja za jioni matokeo yalikuwa bado hayajatangazwa katika wilaya zote hizo na ambapo kwa mujibu wa msimamizi wa uchaguzi wilaya ya Kiteto Bosco Ndunguru alisema matokeo hayo yatatolewa muwa wowote mara baada ya kukamiliswa taratibu zake zikiwemo kujumlisha

Na Sijawa Omary, Mtwara  
15/12/2014
WANACHAMA wa CCM Mkoani Mtwara wametakiwa kutembea kifua mbele kufuatia ushindi wa kishindo waliyoupata katika uchaguzi wa serikali za mitaa uliyofanyika jana nchini kote.


Kwa mujibu wa Katibu wa CCM Mkoa, Shaibu Akwilombe ambaye pia ni Mkurugenzi wa uchaguzi alisema hadi hivi sasa wamepokea matokeo ambayo ccm imeshinda katika vijiji 599 na vyama upinzani 146 katika Mkoa mzima na vijiji 31 matokeo yake bado hayajatangazwa  ambapo  mkoa huo una jumla ya vijiji 777.

Alisema, hapo walipofikia katika nafasi ya vijiji ni sawa na ushindi wa asilimia 77.09% ambapo mkoa huo una vitongoji 3454 na hadi hivi sasa ccm imeshinda katika vitongoji 2192 sawa na silimia 63.46 na pinzani 351 mkoa mzima.

Hata hivyo, wamepata matokeo ya serilikali za mitaa ikiwemo mitaa katika manispaa, wilaya ya masasi na mtwara vijijini ambayo idadi yake ni 179 ambapo ccm wameshinda kwenye mitaa 109 wapinzani mitaa 78 ambapo ushindi huo unawafanya ccm kuwapata ushindi wa 60.90/%.

Pia vijiji wameshinda kwa asilimia 77% ambapo hadi hivi sasa vitongoji 63% na mitaa asilimia 60% .

Akwilombe alisema, wameona ni vema kuwapa taarifa wananchi taarifa kwa kadiri uchaguzi unavyozidi kufikia mwisho ambapo kiuchaguzi wanapozungumzia uchaguzi watu huwa wanashughulika na mtaa au mitaa yao pia kushindwa mtaa mmoja haina maana wameshindwa mkoa mzima.

Aidha, amewashukuru wanamtwara kwa upendo na amani waliyoinyesha katika kipindi hicho cha uchaguzi kutokana hakukuwa na matukio ya ajabu ambapo mikiki mikiki  na rabusha ni sehemu ya mashindano na ni kitu cha kawaida hivyo viongozi na wanasiasa amewataka kuonyesha ukakamavu wao kisiasa ili chaguzi zijazo waweze kufanya katika amani zaidi.

“Kwakweli wanamtwara wameonyesha amani na utulivu wa hali ya juu kwani uchaguzi ulikuwa wa amani na utulivu hakukuwa na vurugu wala hali yeyote ile ambayo ingeweza kuleta uvunjifu wa amani kwani mambo yameenda vizuri napenda niwashukuru wanamtwara kwa hili la kinidhamu ambalo wamelionyesha waendelee na moyo huu hata katika chaguzi zijazo”. Alisema Akwilombe.

Na Richard Mwangulube, Arusha
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) katika jiji la Arusha kimefanikiwa kunyakua mitaa mipya 72 kati ya 154 iliyoshiriki katika uchaguzi wa serikali za mitaa uliofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita.
Hatua hiyo ni ushindi mkubwa kwa chama hicho kilichokuwa kinashikilia mitaa miwili kabla ya uchaguzi huo na kukihenyesha chama tawala cha CCM ambacho kimekuwa kikitawala mitaa hiyo kwa miaka nenda  rudi.
Kwa mujibu wa matokeo yaliyopatikana jana,CCM imeshinda mitaa 78 wakati CHADEMA kikitwa mitaa 75 katika uchaguzi huo.Mtaa mmoja wa Oysterbay katika Kata ya Unga Limited uchaguzi wake unarudiwa kesho (Jumanne)
Katika uchaguzi huo uliokuwa na ushindani mkali na wakati mwingine kuzuka kwa vurugu za hapa na pale,CHADEMA imefanikiwa kuzoa mitaa yote ya kata za Lemara kwa kupara mitaa saba dhidi ya zero ya CCM,Kata ya Terrati imezoa mitaa sita dhidi ya sifuri ya CCM Ngarenaro 5/0,Kimandolu 4/0 huku kikiambulia mtaa mmoja dhidi ya miwili ya CCM katika kata ya Kaloleni. Kwa ujumla Chadema imefanikiwa kushika hata za uongozi katika kata 10 kati ya 25 za Jiji hilo.
Katika kata ya Olorien ambako ndiko nyumbani kwa Meya wa Jiji la Arusha,Gaudence Lyimo(CCM),CHADEMA pia imefanikiwa kuzoa mitaa mitano dhidi ya mmoja wa CCM  huku katika kata ya Sakina ikiongoza kwa mitaa mitano dhidi ya miwili ya CCM
Kata ya Baraa Chadena imezoa mitaa mitano dhidi ya mitatu ya CCM wakati katika kata ya Moivaro imepata mitaa mine dhidi ya miwili ya CCM na Kata ya Moshono Chadema imeshinda mitaa mitano dhidi ya mine wakati Sombetini imeshinda mitaa mitatu dhidi ya mmoja wa CCM,hali ikiwa hiyo hiyo katika Kata ya Osunyai.
Katika uchaguzi huo CCM imefanikiwa kuzoa mitaa yote miwili katika kata ya Mjini Kati na kushinda kwa idadi hiyo katika kata ya Levolosi ambaye diwani wake ni wa Chadema.
CCM imefanikiwa kushinda katika kata ya Murrieti ambako imezoa mitaa 10 dhidi ya mitatu ya Chadema, Kata ya Engutoto imepata mitaa mitano dhidi ya mmoja wa Chadema na imeshinda mitaa 9 dhidi ya minne ya chadema katika kata ya Elerai.
CCM pia imeshinda mitaa mitatu dhidi ya miwili ya chadema katika kata ya Themi,na kushinda kwa idadi hiyo katika kata ya Olasiti huku ikipata ushindi mnono wa mitaa minne  dhidi ya mmoja wa Chadema katika kata ya Olomoti.
Chama hicho tawala pia imepata mitaa mingi katika kata ya Ungalimited ambako ilizoa minne dhidi ya mmoja wa Chadema, kata ya Sekei imepata mitaa minne dhidi ya miwili ya Chadema huku kikishinda mitaa minne dhidi ya mitatu ya Chadema.


Na Ashura  Hussein, Bukoba,
CHAMA  cha mapinduzi  (CCM) Manispaa ya Bukoba Mkoani Kagera wamepoteza  mitaa  20 ambayo  imechukuliwa  na chama cha demokrasia  na maendelo  (CHADEMA ) katika uchaguzi  mdogo wa serikali za mitaa uliofanyika Desemba 14 mwaka huu hivyo kuwa na jumla ya mitaa 35kabla ya uchaguzi  walikuwa na mitaa 55 kati mitaa 66.

Akifanya  mahojiano  na mwandishi wa gazeti   hili  katibu wa chama cha mapinduzi ( CCM ), Manispaa ya Bukoba Abdul Kambuga, alisema katika  uchaguzi huu serikali za mitaa chama  hicho   kimepata viti  35 wakati  kabla   ya uchaguzi walikuwa na viti  55 huku wapinzani ( ukawa )wakiwa na jumla ya viti 11.
Kambunga,alisema  uchaguzi huo umegubikwa  na changamoto mbalimbali ikiwemo  baadhi yawatu kujiandikisha kwenye mitaa wasiyoishi.
Alisema sheria za uchaguzi hazikufuatwa na msimamizi wa uchaguzi wa manispaa kukiuka ibara ya 19 kifungu cha 6 kinachomtaka mpiga kura kuonyesha kitambulisho  na  hawakufanya  hivyo.

Aliongeza  kuwa upigaji kura ulikuwa wa kiholela ndio  maana umesababisha matokeo hayo kwa baadhi ya wenyeviti wa ccm kukosa nafasi na kwenda kwa chadema.
Alipohojiwa  idadi ya wajumbe na viti maalum waliopatikana kwa tiketi  ya (CCM ) alisema hajapata taarifa rasmi.

“mfano Kata ya kashai vijana 2800  waliwekewa pingamizi   likini hakuna    hatua yoyote   iliyochukuliwa na msimamizi  hivyo ni dhahiri kuwa watendaji aliosimamia uchaguzi   walihujumu utaratibu wa kupiga kura”alisema Kambuga.

“naiomba serikali ibatilishe  matokeohaya na kupanga  uchaguzi kufanyika upya”anaongeza katibu.

Kwa  upande  wake    mwenyekiti  wa ( chadema  )manispaa  ya Bukoba Victor Sherejei ,alisema ushindi walioupata  ni wa kishindo.

Sherejei ,alisema kati  ya mitaa 66 ya  manispaa ya Bukoba  chadema wamepata mitaa 29,cuf  2 na ccm wamepata mitaa 35.
Alisema  wajumbe  wa serikali za mitaa na viti maalum kwa manispaa ni 330 kati yao 200 ni wa chadema ,cuf  5 na ccm 125.

Alisema  ushindi huo wa chadema  umetokana na Watanzania kuhitaji kupata mabadiliko  baada ya kuyakosa ndani ya ccm hivyo wanahitaji kuyapata kupitia chadema.

Alipohojiwa  sababu za baadhi ya wenyeviti kuwa wa chama cha mapinduzi huku wajumbe wakiwa ni chadema alisema chama tawala kilielekeza hujuma  upande wa wenyeviti kwa kutoa karatasi tatu za kupigia kura za mwenyekiti kwa watu waliokuwa wamewaanda.
“chadema  tumepata  ushindi wa kishindo ukizingatia tumechukua Mitaa 9 yote ya Kata mama ya Kashai yenye jumla ya wakazi 30,000 kwa mujibu wa sensa iliyofanyika mwaka 2012 “alisema Sherejei.

Aidha  katika wilaya  ya Muleba  inajumla yaVijiji 166 lakini hadi sasa yametangazwa matokeo ya Vijiji 84 ccm 52,chadema 32 huku vijiji 13 ccm wamepita  bila kupingwa. 

Hata  hivyo wilaya  za   Kyerwa na Ngara baadhi ya Mitaa     hawakuweza kufanya uchaguzi kutokana na sababu mbalimbali   ikiwemo vifaa vya kupigia  kura.

Mkurugenzi wa manispaa  ya Bukoba  ambaye  ndiye msimamizi  wa uchaguzi alipotafuta hakupatikana kutoa  matokeo taarifa kutoka ofisini kwake zinasema   yuko  ziara ya mkuu wa mkoa wa Kagera John Mongella ya kujitambulisha.

Na Venance Matinya, Mbeya.
MATOKEO ya awali yaliyopatikana  mkoani Mbeya katika uchaguzi wa Serikali za mitaa unaonesha Chama Cha Mapinduzi(CCM) kuongoza  katika maeneo mengi kikifuatiwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).
Akizungumzia matokeo ya awali,Katibu wa CCM Mkoa wa Mbeya Mwangwi Kundya alisema mpaka anazungumza na waandishi wa habari,matokeo yalipatikana kwenye vitongoji 2047 kati ya 2567, vijiji 606 kati ya 771 na mitaa 252.
Alisema  kwa upande wa vijiji vya Wilaya ya Chunya yenye vijiji 86 yalikuwa yamepatikana matokeo ya vijiji 74, ambapo  kati ya vijiji hivyo,CCM ilikuwa imeshinda vijiji 67 na Chadema vijiji saba.
Wilaya ya Ileje yenye jumla ya vijiji 71 ambapo matokeo yalikuwa yamepatikana ya vijiji 32 CCM ilikuwa imeshinda vijiji 23 na Chadema vijiji 9.
Kwa wilaya ya Kyela yenye jumla ya vijiji 93 ambayo matokeo ya vijiji vyote yalikuwa yamepatikana CCM imeshinda vijiji 79 na Chadema vijiji 13 huku kijiji kimoja uchaguzi ukiwa haukufanyika.
Wilayani Mbarali kuliko na jumla ya vijiji 102, matokeo yalikuwa yamepatikana ya Vijiji 97 ambapo CCM ilikuwa imeshinda katika vijiji 81 na Chadema vijiji 16 na vijiji vitano yalikuwa yakisubiriwa.
Wilaya ya Mbozi yenye vijiji 125 ambapo matokeo ya vijiji 92 yalikuwa yamepatikana CCM ilikuwa imeshinda katika vijiji 84,Chadema vijiji  8 na vijiji 33 yalikuwa yakisubiriwa.
Wilaya ya Rungwe yenye vijiji155,matokeo ya vijiji 150 yalikuwa yamepatikana,CCM ilishinda vijiji 127,Chadema vijiji 22,CUF kijiji kimoja na vijiji vitano matokeo yalikuwa yanasubiriwa.
Wilaya ya Momba ina vijiji 72 kati ya hivyo vijiji 67 yalikuwa yamepatikana,CCM ilikuwa imeshinda katika vijiji 43,Chadema vijiji 24 na vijiji vitano yalikuwa yanasubiriwa.
Kwa upande wa Mitaa Mbeya mjini kuliko na mitaa 181,CCM imeshinda mitaa 106,Chadema mitaa 71 na Nccr Mageuzi mtaa mmoja wakati katika mji mdogo wa Tunduma wilayani Momba ulio na mitaa 71 Chadema iliibuka kidedea katika mitaa 46 na CCM ikaambulia mitaa 25.
Kwa upande wa Vitongoji,Chunya yenye vitongoji 438 ambapo matokeo ya vitongoji 288 yalikuwa yamepatikana,CCM ilikuwa imeshinda vitongoji 270 na Chadema vitongoji 18.
Kyela yenye vitongoji 469 CCM ilikuwa imeshinda vitongoji 377 na Chadema vitongoji 88 huku vitongoji vinne uchaguzi ukiwa unapaswa kurudiwa.
Wilaya ya Mbozi yenye jumla ya vitongoji 664 ambayo matokeo ya vitongoji 414 yalikuwa yamepatikana,CCM ilikuwa imeshinda vitongoji 359,Chadema vitongoji 55 na matokeo ya vitongoji 250 yalikuwa yanasubiriwa.
Wilaya ya Rungwe yenye jumla ya vitongoji 694,matokeo ya vitongoji 634 yalikuwa yamepatikana na CCM ilikuwa imeshinda vitongoji 557,Chadema vitongoji 110,Cuf vitongoji viwili na TLP kitongoji kimoja na vitongoji 60 yalikuwa yakisubiriwa.
Wilaya ya Momba ina jumla ya vitongoji 302 kati ya hivyo vitongoji 242 matokeo yalikuwa yamepatikana ambapo CCM ilikuwa imeshinda 189,Chadema 53 na vitongoji 60 vilikuwa bado matokeo yakisubiriwa.


CCM YAENDELEA KUPETA, CHADEMA YACHUKUA HALMASHAURI YA MJI TUNDUMA NA MAMLAKA YA MJI MBALIZI

Na Moses Ng’wat, Mbeya.
LICHA ya Chama cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Mbeya kikiendelea kupata ushindi katika matokeo ya awali katika uchaguzi wa serikali za mitaa, vyama vya umoja wa Katiba ya wananchi navyo vimeonesha ushindani mkubwa huku vikifanikiwa kushinda na kuunda serikali katika mamlaka mbili za mji.
Kwa mujibu wa matokeo ya awali yaliyotelewa na Katibu wa CCM Mkoa wa Mbeya, Mwangi Kundya, yanaonesha kuwa, chama hicho kimefanikiwa kuzoa idadi kubwa ya vijiji hadi sasa.

Akitangaza matokeo hayo mbele ya waandishi wa habariKundya alisema matokeo ya awali katika Halmashauri ya Jiji la Mbeya lenye mitaa 181, CCM imefanikiwa kupata mitaa 106, Chadema71, NCCR-Mageuzi mmoja.

Wilaya ya Chunya yenye Vijiji 86,ambapo vijiji vilivyokamilisha hesabu ni 74,  CCM ilipata vijiji 67 , Chadema vijiji 7, wakati kwa upande wa vitongoji, CCM ilipata vitongoji 270, huku Chadema ikiambulia vitongoji 18.

Wilaya ya Ileje jumla ya vijiji vyote ni 71 ambapo vijiji 32 vimekamilisha matokeo yake, ambapo CCM imepata vijiji 23, Chadema vijiji 9, ambapo kwa upande wa vitongo….

Wilaya ya Kyela vijiji vyote 93 vimekamilisha matokeo yake, ambapo CCM imepata 79,Chadema 13 , huku uchaguzi wa kijiji kimoja kurudiwa ambapo kwa upande wa vitongoji 469, CCM vitongoji 377, Chadema 88, wakati vitongoji vine uchaguzi kurudiwa.
Wilaya ya Mbarali jumla ya vijiji 102, CCM 81, Chadema 16 ambapo vijiji sita vitafanya uchaguzi wa marudio, ambapo kwa upande wa vitongoji jumla ni 713, ambapo CCM imeshinda vitongoji 570 , Chadema ikiambulia 79 na vitongoji 36 matokeo yake yalikuwa bado.

Wilaya ya Mbozi, vijiji vilivyopo ni 125 ambapo kati ya hivyo 92 matokeo yake yalikuwa tayari ambapo CCM imepata viti 84 na Chadema imepata vijiji nane, huku vijiji 33 matokeo yalikuwa bado, kwa upande wa vitongoji 664, CCM imepata 557 na Chadema 110, CUF viwili, TLP ikiambulia kiti kimoja.

Wilaya Rungwe jumla ya vijiji 155 , CCM imepata 132,Chadema 22, CUF kimoja na vijiji vitano kufanya marudio, wakati upande wa vitongoji vilivyopo ni 694,CCM 578,Chadema 111,CUF 2 na TLP viwili.
Wilaya ya Momba ambayo matokeo yake yamegawanywa katika sehemu mbili kutokana na wilaya kuwa na Halmashauri ya mji wa Tunduma.
Ambapo kwa upande wa vijiji jumla ni 72, CCM imepata vijiji 43,Chadema24 na vijiji vitano kufanyiwa marudio, wakati kwa upande wa vitongoji, jumla ni vitongoji 302, CCM 189, Chadema 53 na vitongoji 60 matokeo yake bado.
Kwa upande wa mitaa katika Halmashauri ya mji wa Tunduma jumla ya mitaa ni 71, CCM imechukua mitaa 25, wakati Chadema imeongoza kwa kupata mitaa 46, hivyo kulazimika kuunda Halmashauri ya mji.
Wakati matokeo ya Wilaya hizo yakipatikana katika mkoa wa Mbeya kwa upande wa Wilaya ya Mbeya Vijijini matokeo ya awali yameshindwa kutolewa kutokana na utata wa hesabu, lakini pia Jografia ya wilaya hiyo kuwa na changamoto ya mpangilio wake.

Hata hivyo, habari za uhakika zinadai kuwa katika uchaguzi wa mamlaka ya mji Mbalizi, CCM imepata vitongoji viwili, huku chadema ikipata vitongoji 10 kati ya 12 hivyo kuwa na uhakika wa kuunda baraza la mamlaka ya mji.

No comments:

Post a Comment