TANGAZO


Thursday, October 9, 2014

Wizara ya Fedha yakutana na uongozi wa Mfuko wa Changamoto za Milenia (MCC) na kujadili jinsi ya kufanikisha Awamu ya Pili ya mfuko huo nchini Tanzania

*Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue ahudhuria mkutano huo
 
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa serikali  Dk. Servacius Likwelile akifurahia jambo na Mkuu wa mambo ya uchumi wa Mfuko wa changamoto za milenia. Wakiwa pamoja na Kamishna wa Fedha za Nje Bw. Saidi Ngosha Magonya.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa Serikali Dk. Servacius Likwelile akifurahia jambo na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi  Ombeni Sefue. Wakishuhudiwa na Bw. Abbas Abeid Missana Mwambata wa uhamiaji Ubalozi wa Marekani wakwanza kutoka kulia na Bw. Laston Msongole ambaye ni Mtendaji Mkuu wa mfuko wa milenia wa awamu ya pili wa mwisho kutoka kulia.
Dk. Servacius Likwelile Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa serikali wakiwa pamoja na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue wakiusikiliza kwa makini ujumbe wa Mfuko wa Changamoto za Milenia.
Ujumbe wa Tanzania ukiwa katika kikao cha majadiliano pamoja na uongozi wa mfuko wa changamoto za Milenia Mjini Washington Dc.Balozi wa Tanzania nchini Marekani – Washington Mhe.Liberata Mulamula pamoja na aliyekuwa Balozi wa zamani wa ubalozi huo Bw. Ombeni Sefue wote walikuwepo katika mjadala huo.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa serikali Dr. Servacius Likwelile wakiwa pamoja na Katibu Mkuu Kiongozi Bw. Ombeni Sefue wakibadilishana mawazo kuhusu mkutano ambao ulianza  muda mfupi baadae katika jengo maarufu la MCC mjini Washington DC. Marekani.
Viongozi wa Mfuko wa Changamoto za Milenia wakimfurahia Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue baada ya kumuona tena na kufurahi kwamba amekuja kujumuika na Watanzania wenzake katika kutafuta fedha za kuinua uchumi wa Tanzania.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa serikali Dk. Servacius Likwelile wakiwa pamoja na Katibu Mkuu Kiongozi  Balozi  Ombeni Sefue pamoja na Balozi Liberata Mulamula wakiusikiliza kwa makini ujumbe wa Mfuko wa Changamoto za Milenia.
Makamu wa Rais wa shughuli za operesheni  za mfuko wa Changamoto za Milenia, Bw. Kamran Khan  wa katikati akitoa maelezo na msimamo wa mfuko huo. Waliomzunguka ni wasaidiki wake ambao anafanya nao kazi kwa karibu.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa serikali Dk. Servacius LikwelileKatibu Mkuu Kiongozi  Balozi  Ombeni Sefue, Balozi Liberata Mulamula pamoja na Bw. Laston Msongole ambaye ni Mtendaji Mkuu wa mfuko wa milenia wa awamu ya pili wakiusikiliza kwa makini ujumbe wa Mfuko wa Changamoto za Milenia na kutoa mawazo yao. (Picha zote na Ingiahedi Mduma- Wizara ya Fedha)

No comments:

Post a Comment