TANGAZO


Saturday, October 11, 2014

Wachezaji wa Timu za Viongozi wa Dini walipotembelea Mbuga ya wanyama ya Mikumi Morogoro

Mwenyekiti wa Kamati ya Viongozi wa Dini, Sheikh Mkuu, Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum, akiwa amepozi kwenye jiwe linaloelezea kuhusu Hifadhi ya Taifa ya Mikumi kwenye lango la kuingilia mbungani humo, wakati viongozi hao, walipotemebelea kujionea wanyama na ndege mbalimbali mbugani baada ya kumaliza kambi yao ya mazoezi, kujiandaa na mpambano wao wa mpira wa miguu utakaofanyika kesho, Uwanja wa Taifa, kabla ya mpambano wa timu ya Taifa Stars na Benin. (Picha zote na Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.com)
Simba wake, wakiwa wamejipumzisha kwenye kivuli cha mti mbugani humo.
Muongoza wageni kwenye Hifadhi ya Taifa ya Mikumi, Hassan Simba, akiwapati maelezo viongozi hao wa dini wakati wakiwa kwenye gari, kuangalia wanyama na ndege mbugani humo.
Tembo wakiwa kwenye kivuli cha mti kujipumzisha.
Twiga wakiwa kwenye kivuli cha mti kwa ajili ya kujikinga jua na kujipumzisha mbugani humo.
Simba dume, akiwa kwenye kivuli cha mti kwa ajili ya kujipumzisha mbugani humo.
Simba jike na dume, wakiwa kwenye kivuli cha mti kwa ajili ya kujikinga jua na kujipumzisha mbugani humo.
Pundamilia wakiwa kwenye kivuli cha mti kwa ajili ya kujikinga jua na kujipumzisha mbugani humo.
  Twiga akila majani ya mti kwenye mbuga hizo.
Viboko wakiwa kwenye moja ya ziwa, wakiwa wamejipumzisha kwenye hifadhi hiyo.
Viongozi wa dini wakiangalia viboko na mamba kwenye ziwa katika hifadhi hiyo ya Mikumi, mkoani Morogoro.
Tembo akila majani kwenye hifadhi hiyo. 
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Sadiki, aliyafuatana na viongozi hao kwenye msafara huo, akionesha jambo baada ya kumaliza kutembelea hifadhi hiyo.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Sadiki, akiwa amekaa kwenye kitanda cha moja ya nyumba za kulala wageni za hifadhi hiyo, alipokwenda kuangalia nyumba hizo, ambazo baadhi ya maharusi baada ya kufunga ndoa zao, huenda kujipumzisha pia wageni mbalimbali nao huamua kujipumzisha kwa kulala kwenye nyumba hizo za hifadhi hiyo.
Viongozi wa dini wakipata chakula cha mchana walichoandaliwa na wenyeji wao, Utawala wa Mkoa Morogoro pamoja na Utawala wa hifadhi hiyo ya Mikumi, mkoani humo.
Sheikh Kwangaya, akihudumiwa vinywaji na Muongoza wageni, Benigna Mwananzila (kushoto) na Mhifadhi Utalii, Tutindaga Mwakijambile (katikati), wakati wa kupata chakula hicho cha mchana.
Viongozi wa dini wakipata chakula cha mchana kilichoandaliwa na wenyeji wao, kwenye hifadhi hiyo ya Mikumi.
Baadhi ya wahudumu wa mambo ya Afya wa viongozi hao wa dini nao wakipata chakula cha mchana.
Viongozi wa dini wakipata chakula cha mchana, kwenye hifadhi hiyo ya Mikumi.
Viongozi wa dini wakipata chakula cha mchana, kwenye hifadhi hiyo ya Mikumi.
Viongozi wa dini wakichukua chakula cha mchana, kilichoandaliwa na wenyeji wao, kwenye hifadhi hiyo ya Mikumi.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Sadiki, akizungumza na vongozi hao pamoja na viongozi na wafanyakazi wa hifadhi hiyo, mara baada ya kupata chakula cha mchana. 
Baadhi ya viongozi hao wa dini wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Sadiki, alipokuwa akizungumza nao.
Baadhi ya viongozi hao wa dini na pamoja na wafanyakazi wa hifadhi hiyo, wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, alipokuwa akizungumza nao.
Baadhi ya viongozi hao wa dini na pamoja na wafanyakazi wa hifadhi hiyo, wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Sadiki, alipokuwa akizungumza nao.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Sadiki, viongozi wa dini na wafanyakazi wa hifadhi hiyo, wakiomba dua mara baada ya mkuu huyo wa mkoa, kuzungumza nao. 
Picha ya pamoja, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Sadiki (katikati), akiwa pamoja na viongozi wa dini, viongozi wa Mkoa wa Morogoro, viongozi na wafanyakazi wa Hifadhi ya Mikumi, wakati wa kuagana tayari kwa viongozi hao kuondoka kwenye hifadhi hiyo.

No comments:

Post a Comment