TANGAZO


Thursday, October 9, 2014

Mashindano ya SHIMIWI yafikia hatua ya Nusu Fainali mjini Morogoro

Timu ya kuvuta kamba ya wanawake ya Ikulu wakiwavuta timu ya Wizara ya Kilimo, Ushirika na Chakula (hawapo pichani) wakati wa mashindano ya kuingia hatua ya nusu fainali mashindano ya SHIMIWI  leo mjini Morogoro ambapo Ikulu imefuzu kucheza hatua hiyo.
Timu ya kuvuta kamba ya wanaume ya Ikulu wakiwavuta timu ya Wakala wa Hifadhi ya Chakula ya Taifa (NFRA- hawapo pichani) wakati wa mashindano ya kuingia hatua ya nusu fainali mashindano ya SHIMIWI leo mjini Morogoro ambapo Ikulu imefuzu kucheza hatua hiyo.
Mshindi wa kwanza wa mchezo wa drafti wanaume Salumu Simba (kushoto) kutoka RAS Dodoma akichuana na mshindi wa tatu wa mchezo huo Ramadhani Mtenga (kulia)kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo wakati wa mashindano ya SHIMIWI leo mjini Morogoro.
Mshindi wa kwanza wa mchezo wa drafti wanaume Salumu Simba (kulia) kutoka RAS Dodoma akichuana na mshindi wa tatu wa mchezo huo Dkt. Idris Lukindo (kushoto) wakati wa mashindano ya SHIMIWI leo mjini Morogoro. 
Baadhi ya watumishi wanaoshabikia mchezo wa drafti wakishuhudia pambano la kuwatafuta  washindi wa mcheo huo  leo katika kiwanja cha Jamhuri mjini Morogoro.
Mchezaji wa timu ya mpira wa pete Ikulu Mwadawa Twalibu (GA) akimiliki mpira wakati wa mchezo wa robo fainali kati ya timu ya Ikulu na Bunge wa kumsaka mshindi atakayecheza nusu fainali, timu ya Ikulu imefuzu kwa kuwashinda timu ya Bunge kwa magoli 67 kwa 24. 
Wachezaji wa timu ya mpira wa miguu ya Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo (waliovalia sare ya bluu) wakisalimiana na wachezaji wa mchezo huo kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu (waliovalia sare ya rangi ya machungwa) kabla ya mchezo wa robo fainali ambapo timu ya Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo wameibuka washindi na kuingia nusu fainali katika mshindano ya SHIMIWI kwa kuifunga timu ya Ofisi ya Waziri Mkuu 1- 0
Timu ya mpira wa miguu ya Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo (kushoto) na timu ya Ofisi ya Waziri Mkuu (kulia) wakiomba dua kabla ya mchezo wa hatua ya robo fainali leo mjini Morogoro.
Baadhi ya watumishi wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo wakishangilia ushindi wa timu yao wa kuifunga timu ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa goli 1- 0 leo mjini Morogoro.  (Picha zote na Eleuteri Mangi- MAELEZO)

No comments:

Post a Comment