TANGAZO


Wednesday, July 30, 2014

Waziri Membe: Dini ndiko kwenye chimbuko la Amani na Utulivu

*Achangia kitabu kilichoandikwa na Mufti 


Habari katika picha kuhusu Baraza la Eid el Fitri

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Kamilius Membe, akizungumza jambo na Waziri Mkuu Mstaafu, Dk. Salim Ahmed Salim, huku waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye (kulia) akifuatilia mazungumzo hayo kwa pembeni, wakati wakiwa kwenye hafla ya Baraza la Idd El Fitri jana, Julai 29, 2014, kwenye Viwanja vya Kariamjee, Jijini Dar es Salaam.
Mgeni rasmi kwenye Baraza la Eid ElFitr, Waziri Mkuu Mizengo Pinda, akiingia kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam, akisindikizwa na  Sheikh wa mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum.
 Pinda akimsalimia Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi baada ya kuwasili ukumbini
Waziri Mkuu Mizengo Pinda akimsalimia Mufti wa Tanzania, Sheikh Mkuu, Shaaban Issa Simba baada ya kuwasili ukumbini.
Pinda akimtazama kwa furaha wakati Mwinyi akizindua kitabu kwa furaha ambacho kimeandikwa na Sheikh Mkuu, Shaaba Issa Simba, kitabu hicho chenye jina la Al Muhtaswar ni makusanyo mbalimbali ambayo sheikh Mkuu huyo ameyakusanya na kisha kutengeneza kitambu kwa ajili ya kukisambaza nchini kote kusaidia waislam kuzingatia vyema dini hiyo. Pamoja na wadau kadhaa, Waziri wa Mambo ya Nje Bernard Membe amechangia kuwezesha uchapishaji wa kitabu hicho.
 Mtoto  wa jijini Dar es Salaam, Arafat Msham akidurusu kitabu hicho.
Waziri Membe, Dk. Salim na Sumaye wakisoma kitabu cha Sheikh Mkuu Shaaban Issa Bin Simba
 Waziri Mkuu Mizengo Pinda akitoa hotuba yake kwenye Baraza hilo la Idd
 Akinamama kwenye Baraza hilo la Eid El Fitri.
Mke wa Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda (kulia) akiwa na Mama Shamim Khan kwenye Baraza hilo la Eid. 
Kijana wa Madrasa, akighani kaswida maalum kwenye baraza hilo, la Idd
Vijana wa Madrasa, wakitumbuiza kwa kaswida kwenye Baraza la Idd el Fitri.
Ustaadhi Mroki Mroki wa Habari leo na Mkurugenzi Mwendeshaji wa Blogu ya Father Kidevu, akifuatilia kwa makini shughuli za hafla hiyo, ya Baraza la Eid el Fitri.
Baadhi ya wasanii maarufu wa Bongo Movie, akiwemo Steve Nyerere, nao walihudhuria baraza hilo.
Membe akiagana na wadau baada ya shughuli za Baraza la Eid el Fitri. (Picha zote kwa hisani ya Bashir Nkoromo-the Nkoromo Blog)

No comments:

Post a Comment