TANGAZO


Sunday, July 28, 2013

KCB Benki yatoa Mashine ya ultrasound Hospitali ya Kanisa la Wasabato (SDA) jijini Mwanza kusaidia maelfu ya wazazi Kanda ya Ziwa

Meneja wa benki ya KCB tawi la Mwanza, Joseph Njile (kushoto) akikabidhi mashine ya kisasa ya ultrasound kwa mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya ya Ilemela, Amina Masenza (kulia), kabla ya kuikabidhi kwa uongozi wa Hospitali ya SDA ya jijini Mwanza. Mashine hiyo yenye thamani ya shilingi milioni 15 ni mahsusi kwa kupima afya ya wajawazito ili kuwawezesha wapate uzazi salama.


Mtaalamu  wa mashine za Ultrasound, Dk. Joseph Kajiru akijipima yeye mwenyewe kwa kutumia mashine ya ultrasound ili kuhakiki utendaji wa mashine hiyo ya kidijitali iliyotolewa kama masaada na benki ya KCB kwa Hospitali ya wasabato ya jijini Mwanza.


Mtaalamu  wa mashine za Ultrasound, Dk. Joseph Kajiru akijipima yeye mwenyewe kwa kutumia mashine ya ultrasound ili kuiangalia utendaji wake wa kazi. 

Mtaalamu wa mashine ya Ultrasound, Dk. Kajiru akionyesha picha na matokeo ya uchunguzi uliofanywa na mashine ya ultrasound iliyotolewa mwishoni mwa juma na benki ya KCB kwa hospitali ya Wasabato ya jijini Mwanza.
Mtaalamu  wa mashine za Ultrasound, Dk. Joseph Kajiru akiingalia masheni hiyo mara baada ya kukabidhiwa na benki hiyo ya KCB jijini Mwanza mwishoni mwa wiki.

Na Mwandishi, Mwanza
Benki ya KCB tawi la Mwanza  imetoa msaada wa mashine ya kisasa ya na vifaa vengine vya upimaji  kwa kwa hospitali ya  Kanisa la Wasabato (SDA) ya  jijini hapa ikiwa ni azma yake  kuboresha uzazi salama katika mikoa ya Kanda ya ziwa.


Msaada huo ambao uliambatana na mashine ya kuchapa matokeo papo hapo, ulitolewa mwishoni mwa juma kwa hospitali hiyo na meneja wa KCB tawi la Mwanza, Joseph Njile mbele ya Mkuu wa Wilaya ya Ilemema , Amina Masenza na Askofu Mkuu wa jimbo la Nyanza, Joseph Bulengela.


"Mashine na vifaa hivi ni mahsusi  kwa upimaji na utoaji wa matokeo papo hapo kwa wajawazito na wagonjwa wengine wenye matatizo ya tumbo, uzazi, kansa na  udhaifu wa viungo vya ndani, kwa mwaka mzima, mashine hizi zinaweza kuhudumia zaidi ya watu 3,000,"  alisema Daktari Joseph Kajiru, Mganga Mfawizi wa hospitali hiyo.


Kwa upande wake, meneja wa KCB tawi la Mwanza,  Bw Njile alisema vifaa vya kidijitali vilivotolewa na benki yake vina jumla ya thamani ya shilingi milioni 15 ikiwa ni kutekeleza ahadi ya benki yake kwa wananchi wa Mwanza ambayo ilitolewa  mwaka jana wakati wa ziara ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,  Uratibu na Mahusiano, Steven Wassira.


  "Mimi nafarijika sana kusikia  kwamba mashine mpya imefika kwa wakati muafaka na iko tayari kuanza kutumiwa  mara moja," alisema Bw Njile katika hafla iliyohudhuriwa pia na mamia ya waumini wa madehehebu ya Kisabato jijii.


Mmoja wa wakazi wanategemewa kunufaika na ujio wa mashine hizo, alikuwa ni mjamzito aitwaye Adela Misana, 28,  ambaye  alidai kuwa  mashine hizo za kisasa zimempa yeye  na akima mama wengine  uhakika wa uzazi salama ambao utaepusha vifo vya wazazi na watoto wakati wa kujifungua.


"Mimi namshukuru Mungu kwa kuipa KCB moyo wa huruma na upendo  kwani mashine hii  itawapa ufanisi mkubwa  wafanyakazi wa hospitali katika kufuatilia afya za wajawazito  na hatimaye kuwawezesha wapate uzazi salama," alisema mama huyo mwenye watoto wawili.


Zaidi ya hayo, Askofu mkuu wa Jimbo la Nyanza,  Bulengela alitoa shukrani zake kwa KCB kwa msaada wa vifaa tiba vitakavyookoa maisha ya maelfu na kutoa wito kwa mamlaka ya hospitali kuvitunza vifaa hivyo ili viendelee kuhuduia watu kwa muda mrefu.


 "Mchango mkubwa ambao thamani yake ni zaidi ya Shilingi milioni 15 zilizotumika kwa ununuzi wake kwa sababu thamani ya uhai wa binadamu haipimiki kwa fedha,"

Kwa kumalizia meneja wa tawi bwana Njile, alisema: "Itakuwa faraja kubwa kusikia kuwa akina mama na wajawazito  mkoani Mwanza na kanda ya ziwa kwa ujumla wamepata mafanikio makubwa ya kiafya kupitia hospitali hii na vifaa ambavo KCB imevikabidhi leo hapa."

No comments:

Post a Comment