TANGAZO


Monday, July 22, 2013

Chama cha Msalaba Mwekundu Tanzania kugawa vyandarua 68,000 Kambi ya Wakimbizi ya Nyarugusu, Kigoma

CHAMA CH


Rais wa Chama cha Msalaba Mwekundu Tanzania 
(TRCS), Dk. George Nangale (kushoto), akizungumza 
katika mkutano na waandishi wa habari Makao Makuu ya chama hicho Dar es Salaam leo, kuhusu uzinduzi wa ugawaji wa vyandarua 68,000 utakaofanyika katika Kambi ya Wakimbizi ya Nyarugusu mkoani Kigoma Julai 30 mwaka huu. Kulia ni Mkurugenzi wa Huduma ya Afya wa chama hicho, Bertha Mlay.

 Ofisa Uhusiano na Mawasiliano wa TRCS Raymond Kanyambo (kushoto), akimkaribisha Rais wa Chama cha Msalaba Mwekundu Tanzania (TRCS), Dk. George Nangale na viongozi wengine kwenye mkutano huo
 Mgurugenzi wa Huduma na Afya wa TRCS Bartha Mlay akijitambusha mbele ya wanahabari.Kushoto ni Makamu Rais wa Chama hicho, Dk.Zainabu Gama na Rais wa chama hicho Dk.George Nangale.
 Mpiga picha wa gazeti la Habari Leo Mroki Mroki akiwa kazini kwenye mkutano huo.
 Mkazi wa Tandale kwa Tumbo Amina Mwalimu akitoa ushuhuda mbele ya wanahabri jinsi alivyonufaika na mataumizi ya vyandarua vilivyoweka dawa vinagaiwa na TRCS.
 Rais wa TRCS, Dk.George Nangale akiteta jambo na  Mgurugenzi wa Huduma na Afya wa TRCS Bartha Mlay.
 Maofisa wa TRCS wakiwa kwenye mkutano huo.


 Rais wa Chama cha Msalaba Mwekundu Tanzania (TRCS), Dk. George Nangale (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Makao Makuu ya chama hicho Dar es Salaam leo, kuhusu uzinduzi wa ugawaji wa vyandarua 68,000 utakaofanyika katika Kambi ya Wakimbizi ya Nyarugusu mkoani Kigoma Julai 30 mwaka huu. Kushoto ni Makamu wake Dk.Zainabu Gama.
 Rais wa Chama cha Msalaba Mwekundu Tanzania (TRCS), Dk. George Nangale (katikati),akizungumza katika mkutano huo. Kulia ni Mgurugenzi wa Huduma na Afya wa TRCS Bartha Mlay na Makamu wa Rais wa TRCS Dk. Zainabu Gama.
Makamu wa Rais wa TRCS Dk. Zainabu Gama akichangia jambo katika mkutano huo. Kulia ni Mkurugenzi wa Huduma na Afya wa TRCS, Bertha Mlay na Rais wa TRCS Dk. George Nangale.
Wanahabari wakiwa kwenye mkutano huo.

Na Dotto Mwaibale

CHAMA Cha Msalaba Mwekundu Tanzania (TRCS), kimedhamiria kutokomeza ugonjwa wa malaria kwa kugawa vyandarua 68,000 katika kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu, iliyopo mkoani Kigoma.

Wakati huo huo, imeelezwa kuwa watu 700,000 kila mwaka wanafariki kutokana na ugonjwa wa malaria na endapo tahadhari isipochukuliwa idadi hiyo itazidi kuongezeka.

Akizungumza na waandishi wa habari Makao Makuu ya chama hicho jijini Dar es Salaam leo Rais wa Chama hicho, Dk.George Nangale alisema kutokana na kukithiri kwa ugonjwa huo chama hicho kimedhamiria kutokomeza malaria kwa kugawa vyandarua vyenye dawa 68,000 katika kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu iliyopo Kigoma.

Alisema katika muendelezo wa shughuli za uzuiaji maambukizo ya malaria Julai 30 mwaka huu, watazindua kampeni ya ugawaji vyandarua hivyo ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Mkuu wa mkoa huo.

Aliongeza kuwa Julai 31, mwaka huu itafanyika shughuli ya ugawaji vyandarua hivyo ambapo wakimbizi wawili watapata chandarua kimoja.

"Shughuli hii imelenga zaidi kuwasaidia watoto na wajawazito kwani tunatambua umuhimu wa vyandarua na jinsi wanavyoathirika na ugonjwa huu,"alisema Dk.Nangale.

Aliongeza kuwa msaada huo umetokana na taasisi mbalimbali, serikali kwa kushirikiana na taasisi ya Umoja wa Mataifa (USAID) ambapo kauli mbiu ya mradi huo ni Hakuna bali vyandarua.

Dk.Nangale alisema kuwa pia wadau 118 watashiriki ambapo hadi sasa chama hicho kimegawa vyandarua Mil.16.5 nchi nzima na kuwalinda zaidi ya watu Mil 29.7 ambapo pia watu 490,000 walikufa kwa ugonjwa huo.

 Alisema mkakati wao hadi itakapofika mwaka 2015 ugonjwa huo uwe umebaki historia.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Huduma ya Afya wa chama hicho, Bertha Mlay alisema kwa mwaka huu wamegawa vyandarua 5,010,000 vyenye dawa katika mikoa ya Lindi, Mtwara na Ruvuma ambao walionufaika ni wanafunzi wa shule za msingi na sekondari.

Pia kwa mwaka jana Visiwani Zanzibar waligawa vyandarua 650,000 kwa ufadhili wa USAID na Grobal Fund.

"Vyandarua tunavyotoa tunahakikisha vina ubora na vinafaa kwa matumizi ya binadamu na ni muhimu kwa jamii kuona umuhimu wa kutumia vyandarua hivi kwa matumizi sahihi na kuachana na matumizi yasiyofaa,"alisema Mlay.

Naye Kaimu Rais wa chama hicho, Dk.Zainab Gama alisema ugonjwa huo umekuwa tishio kwa nchi sita zikiwemo Tanzania,Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo (DRC), Burundi ambapo inakadiriwa kwa mwaka huu watu 11,000 wakiwemo wajawazito na watoto chini ya umri wa miaka mitano walilipotiwa kuumwa ugonjwa huo sawa na asilimia 60.

Mkazi wa Tandale kwa Tumbo Amina Mwalimu alimeishauri jamii izingatie matumizi sahihi ya vyandarua kwani zinasaidia kutokomeza ugonjwa wa malaria.

Alisema hapo awali yeye pamoja na familia yake walikuwa wakishambulia na ugonjwa wa malaria lakini tangu waanze kutumia vyandarua hivyo tatizo hilo limekwisha kabisa.

Aliongeza kuwa ni vyema jamii ikafahamu umuhimu wa vyandarua na kupunguza maradhi yanayozikumba familia nyingi kutokana na kutotumia vyandarua.

No comments:

Post a Comment