TANGAZO


Thursday, September 6, 2012

Rais Kikwete atunukiwa tuzo ya Uongozi Bora katika Sera za Kilimo na Chakula


 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikabidhiwa Tuzo ya Uongozi Bora wa Sera ya Kilimo na Chakula toka kwa Ajay Vashee, Makamu Mwenyekiti wa asasi isiyo ya Kiserikali inayohusika na Sera za Kilimo, Chakula na Maliasili, ijulikanayo kama Food, Agriculture and Natural Resources Policy (FANRPAN), Hoteli ya White Sands, Dar es Salaam jana Septemba 5, 2012. Anayeshuhudia kulia ni Katibu Mtendaji wa FANRPAN), Dk. Lindiwe Sibanda. Tuzo hiyo, ambayo hutolewa kwa kiongozi aliyefanya juhudi kuhakikisha kuwepo kwa Sera bora za kilimo na chakula nchini kwake, ilichukuliwa na Malkia Ntombi Indlovukazi wa Swaziland mwaka jana, wakati Rais Hifikepunye Pohamba alitunukiwa mwaka 2010, Rais Armando Emilio Gwebuza mwaka 2009 na Rais wa Malawi, Hayati Bingu Wa Mutharika, aliipokea mwaka 2008.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifurahia tuzo hiyo, aliyokabidhiwa na Makamu Mwenyekiti wa asasi isiyo ya Kiserikali inayohusika na Sera za Kilimo, Chakula na Maliasili, ijulikanayo kama Food, Agriculture and Natural Resources Policy (FANRPAN), Ajay Vashee, Hoteli ya White Sands, Dar es Salaam jana Septemba 5, 2012. 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikabidhiwa hati ya kutambua mchango wake huo na Makamu Mwenyekiti wa asasi isiyo ya Kiserikali inayohusika na Sera za Kilimo, Chakula na Maliasili, ijulikanayo kama Food, Agriculture and Natural Resources Policy (FANRPAN), Ajay Vashee, Hoteli ya White Sands, Dar es Salaam jana Septemba 5, 2012. 
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiangalia baadhi ya ng'ombe, anaowafuga kwa kufuata njia za kisasa kwenye shamba lake, kijijini kwake Msoga, Chalinze, Wilaya ya Bagamoyo, leo Septemba 6, 2012.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwaangalia baadhi ya ng'ombe hao, anaowafuga kwa kufuata njia za kisasa kwenye shamba lake, kijijini kwake Msoga, Chalinze, Wilaya ya Bagamoyo leo. (Picha zote na Ikulu)

No comments:

Post a Comment